Rais wa Shirikisho la Muziki nchini Addo Novemba akiwa na Katibu mkuu wa Shirikisho hilo Siza Mazongera,na viongozi wengine wa vyama vya muziki  wakizungumza na Wanahabari Leo Agosti 18,2023 wakati akitangaza ujio wa Tamasha kubwa la muziki litakaloshirikisha vyama vyote vya muziki nchini

*Shirikisho la Muziki latarajia kufanya Tamasha 2023*

Na.Khadija Seif,Michuziblog
SHIRIKISHO la Muziki Tanzania (TMF) limelaani vikali vitendo vya wanamuziki wanaotunga nyimbo zinazokashifu uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na uwekezaji wa bandari.


Akizungumza na Wanahabari Leo Agosti 18,2023 Jijini Dar ar es Salaam wakati akitambulisha ujio wa tamasha la muziki kubwa nchini, Rais wa Shirikisho la Muziki (TMF) Addo Novemba amesema wasanii wanapaswa kutunga nyimbo ambazo zinahamasisha amani na kumpongeza Rais Dkt. Samia kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi na kuhakikisha wasanii katika tasnia zote nchini wanafanya kazi katika mazingira yanayoshawishi wawekezaji kutokana na kuweka Mfuko wa wasanii wakukopeshwa fedha.

"Wasanii wanapaswa tumia vipaji vyao katika kuandika nyimbo zenye maadili ya kuonya, kukataza na kuelimisha, kwa sababu sasa hii ndio tasnia inayowasilisha jumbe zake kwa njia ya nyimbo na tungependa sana kama Shirikisho tuweze kukutana na Rais wetu Mama yetu Dkt.Samia SuluhuHassan tuweze kuzungumza nae hiyo ndio kilio chetu."

Aidha, Novemba ameeleza mikakati ya Shirikisho hilo ni kuhakikisha wasanii wote wanashiriki Tamasha hilo linalokwenda kuwaweka pamoja.

"Moja ya mikakati yetu ni kuandaa tamasha kubwa ambalo litawakutanisha wasanii wachanga na wakongwe,

Pia, Novemba ameeleza mkakati mwingine ni kuwa karibu na vyombo vya habari katika kuhakikisha muziki unapata fursa ya kupenya kwa watu kutoka sehemu mbalimbali.

"Kumekuwa na matamasha mbalimbali lakini Shirikisho la muziki tumeamua kuandaa Tamasha letu, pia tunatamani kukutana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tumeona anakutana na watu tofauti, wakati wake kukutana na shirikisho."

Kwa upande katibu Msaidizi wa Shirikisho la Muziki (TMF) Farid kubanda a.k.a Fid Q amesema ni wakati sasa Wanahabari na vyombo vya habari kuwapa nafasi(airtime) wasanii wanaotunga nyimbo kuhamasisha amani au kuhimiza jambo lenye tija katika jamii badala yake kufanya utafiti kwenye nyimbo ambazo jamii hazifaidiki nazo zaidi ya kuleta mmomonyoko wa maadili na desturi za kitanzania.

"Wanahabari wamekuwa wakipoteza muda kuhakikisha nyimbo zenye lugha mbovu zinapewa nafasi kusikika maredioni au hata msanii aliyetunga nyimbo hiyo kufanyiwa Mahojiano wakati waliofanya kazi nzuri hawapatiwi muda huo."

Caption:0Rais wa Shirikisho la Muziki nchini Addo Novemba akiwa na Katibu mkuu wa Shirikisho hilo Siza Mazongera,na viongozi wa vyama wakizungumza na Wanahabari Leo Agosti 18,2023 wakati akitangaza ujio wa Tamasha kubwa la muziki litakaloshirikisha vyama vyote vya muziki nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...