Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inashiriki  katika maonyesho ya 95 ya Kilimo na Biashara yanayofanyika Lusaka Nchini Zambia.

TPA inashiriki katika maonyesho hayo kama moja ya Kampeni za Kimasoko na Elimu kwa Umma na Wadau zenye lengo la kutangaza Huduma za TPA ili kuongeza idadi ya Wateja na kiwango cha Shehena katika Bandari za TPA

Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametembelea Banda la TPA katika maonesho hayo.

Balozi Mkingule ameipongeza TPA kwa kudhamini na kushiriki katika maonyesho hayo na kutoa wito kwa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini Zambia na Nchi za SADC kuendelea  kutumia Bandari za Tanzania na hasa Bandari kuu ya Dar es Salaam  ambayo ina mchango mkubwa katika Sekta ya Uchukuzi kwa Tanzania na Nchi jirani ikiwemo Zambia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...