Na Mwandishi wetu Dodoma

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Standi(VETA) kwa kushirikiana na Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) kupitia programu ya Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Africa(E4D) imeandaa Kongamano la Ajira linalotarajiwa kufanyika tarehe 24 Agosti, 2023 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Abdallah Ngodu kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Veta huku akisema kongamano hilo litakuwa na maonesho ya kujenga uelewa juu ya fursa za ufundi stadi zilizopo kwenye mradi ili kukuza uwezo wa kuajirika kwa wahitimu au wanufaika wa kozi zinazotolewa na Vyuo vya VETA.

''Vilevile kupitia kongamano hilo wanafunzi/wanafaika watakutanishwa na waajiri ili waweze kushirikishana kuhusu taarifa za soko la ajira''amesema

Aidha amesema utekelezaji wa Mradi wa E4D unahusisha ushiriki wa viwanda ambapo mpaka sasa viwanda na makampuni zaidi ya 20 yamethibisha kushiriki na kuonesha huduma na bidhaa zao kupitia kongamano hilo.

'' Tunaamini kuwa makampuni pia yatapata fursa muhimu ya kuthibitishwa kwa uhalisia kuhusu umahiri na ujuzi wa wahitimu na wanufaika wa mafunzo ya ufundi stadi ili wajenge imani na hatimaye kuwapatia fursa za ajira vijana hao''amesema

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Cha ufundi Cha  Veta Dodoma STANSLAUS NTIBARA,amesema hadi kufikia tarehe 19 mwezi huu  jumla ya wanafunzi 1806  wa Mkoa wa Dodoma waliokuwa wameshahitimu mafunzo hayo.

Naye Mwakilishi Mshauri wa programu kutoka Shirika la GOPA,  Bi, LEAH DOTTO, amesema mradi huo  unalenga kuwaandaa vijana kupata ajira kwenye uwekezaji ambao unafanyika hapa nchini na kuweza kujiajiri .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...