Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Kiwanda
cha kutengeneza Marumaru cha KEDA kilichopo Chalinze, Mkoani Pwani,
kimetoa Boksi 1,750 zenye thamani ya sh.milioni 46 ikiwa ni mchango kwa
shule za sekondari za Jakaya Mrisho Kikwete na Miono High School
zilizopo halmashauri ya Chalinze.
Akiwashukuru
wahisani hao, Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambae pia ni Naibu Waziri wa
Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amewaasa wananchi kutunza
miundombinu ya elimu ili kudumisha shule hizo.
Alieleza, ushirikiano na wadau mbalimbali utachochea maendeleo katika kuboresha shule zetu.
Ridhiwani
anasema , Serikali inafanya kwa uwezo wake mkubwa kutenga fedha za
kujenga miundombinu mbalimbali Lakini kwa juhudi za wadau kuongeza
ushirikiano wao itasaidia kusukuma maendeleo ya sekta ya elimu.
#KaziInaendelea #Keda #Elimu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...