Na Fauzia Mussa


Wakulima wameshauriwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo kupata mikopo na elimu ili kuboresha kilimo chao.

Akizungumza wakati akifungua semina fupi ya wakulima,wafugaji na wavuvi katika Viwanja vya maonesho ya Wakulima Dole Mkurugenzi Idara ya Kilimo na uhakika wa Chakula Hamad Masoud Ali amesema wakulima hao wamekua wakishindwa kufikia malengo kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kukiboresha kilimo.

Aidha amesema kuwa wakulima wengi wa Zanzibar wamejikita katika kilimo cha kujikimu (chakula) hivyo uwepo wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Visiwani kutawasaidia wakulima hao kutoka katika kilimo cha zamani na kuweza kulima kisasa.

Alielezea kuwa Semina hiyo itawasaidia wakulima kujua fursa mbali mbali zinazopatikana katika benki hiyo ,hivyo amewataka wadau hao wa kilimo kuwa watulivu na wasikivu ili kupata elimu ya kutosha ili kuleta mabadiliko ya kilimo Nchini.

Hata hivyo Mkurugenzi Hamad aliwasisitiza wakulima hao kuchukua mikopo na kuitumia katika malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kununua mbegu bora,dhana za kulimia na mbolea za kisasa ili kupata mazao yenye tija.

"tumieni fursa hii benki imeshakuja kopeni nunueni matrekta muachane na vijembe vidogo,nunueni mbegu bora ,pamoja na mbolea ili kupata mazao mengi na faida zaidi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla"alifahamisha Mkurugenzi

Mapema aliwataka wajumbe wa semina hiyo kuwa mabalozi wazuri kwa wakulima wengine na kuwataka kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia benki hiyo.

Nae Afisa Maendeleo ya Biashara Mkuu Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB kanda ya Zanzibar Ashura Akim amesema Tasisi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwapatia wakulima, wavuvi na wafugaji mikopo itakayowatoa katika kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha biashara

vile vile alisema kuwa taasisi hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia wakulima kuweza kulifanya Taifa kuwa na chakula timilifu hivyo aliwataka wakulima hao kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo ya muda mrefu,mfupi na muda wakati.

"kilimo ndio uti wa Mgongo wa Taifa ,hili ndilo limetusukuma kuleta huduma zetu Visiwani nawashauri mujiunge kwenye vikundi ili muweze kutambulika na kuipata fursa hii.

akizungumzia suala la riba katika mikopo hiyo Afisa huyo amesema taasisi inatoza asilimia 10 ya riba katika mkopo na wapo katika harakati za kupata leseni ya islamic bank ili kuweza kuwadhamini wakulima ambao hawahitaji mkopo ulio na riba.

Alifahamisha kuwa katika kuhakikisha kilimo kinaendelea , na wakulima wanaachana na kilimo cha kutegemea Mvua benki hiyo inatoa mikopo ya vifaa kama trekta,mashine za maji ,maziwa na kusindikia samaki.

akizungumzia baadhi ya masharti ya mkulima kuweza kupata Mkopo huo amesema kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mkulima amelima alau kwa misimu miwili na kuwa amejisali katika vikundi vinavyotambulika.

aidha alifahamisha kuwa benki hiyo imekuwa ikishirikaina bega kwa bega na serikali kuweza kupata mabwana shamba wa kuwapatia elimu wakulima juu ya mbinu bora za kulima kilimo chenye tija .

Mkuu wa kitengo cha Wakulima Mstaafu Othman Ali Maulid amesema wakulima wa Zanzibar wanauhitaji mkubwa wa rasilimali fedha hivyo uwepo wa benki ya maendeleo ya kilimo visiwani kutawanyanyua wakulima hao na kujikomboa kiuchumi.

Vile vile alisema kupitia benki hiyo wanatarajia mageuzi makubwa kwa wakulima wadogo wadogo kwa kuweza kulima ,kuvua na kufuga kibiashara na kukifanya kilimo hicho kua na tija na kuchangia usalama wa chakula katika Nchi.

amesema wakulima walio wengi wa Zanzibar ni wakulima wenye hali za chini hivyo kuweka masharti magumu kama kuweka hati za nyumba na mashamba wakati wa kupatiwa mkopo huo kutakwamisha juhudi zao za kutaka kupiga hatua za kimaendeleo kupitia kilimo.

Nao washiriki wa semina hiyo wameiomba benki ya maendeleo ya kilimo kuweka masharti nafuu ya mkopo kwani huko nyuma wakulima wengi walishindwa kupata mkopo kutokana na kutokukidhi masharti .

Waliongeza kuwa miongoni mwa faida za kuwepo maonesho ni pamoja na wananchi kupata elimu kuhusiana na mambo mbalimbali hivyo waliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata fursa kama hizo.

Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB ni Taasissi inayomilikiwa na Serikli ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2015 ikiwa na lengo la kuwapatia mikopo wakulima, wavuvi , wafugaji na watu wote wanaojihusisha na kuyaongeza thamamani mazao yanayotokana na kilimo,Ufugaji na Uvuvi.
Bwana Shamba kutoka Wizara ya Kilimo Makame akitoa elimu ya mbogamboga kwa wananchi waliojitokeza kutembelea mabanda ya maonesho ya kilimo yanaendelea huko Dole Wilaya ya Magharibi A

Wananchi mbali mbali wakitembelea mabanda ya maonesho ya kilimo yanayoendelea huko Dole Wilaya ya Magaharibi A.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...