WAKAZI wa kijiji cha Mandepwende na kitongoji cha Zanzibar kata ya Lwinga wilaya ya Namtumbo wameishukuru serikali kupitia wakala wa Barabara za mijini na vijijini(Tarura) wilayani humo kukamilisha ujenzi wa daraja katika mto  Kotoko ambalo limechochea uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.


Wamesema,kukamilika kwa 
daraja hilo na ufunguzi wa Barabara mpya inayounganisha kijiji hicho na maeneo ya uzalishaji,hivyo kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani kwenda sokoni na kufanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato.


Hasibuna Lutumbo makzi wa 
Mandepwende alisema,kabla ya kujengwa daraja la Kotoko changamoto kubwa ilikuwa namna ya kupita katika eneo hilo kwenda upande wa pili kwani wakati wa masika ujaa maji na hivyo kuwa vigumu kwenda maeneo mengine kufuata huduma muhimu za kijamii.


Aidha alisema,kukosekana kwa  
Barabara ya uhakika kwa muda mrefu,kumechangia kuongezeka kwa  umaskini miongoni mwao licha ya jitihada kubwa wanazofanya  za uzalishaji.


“tunaishukuru sana serikali 
yetu ya awamu ya sita kupitia Tarura kukamilisha ujenzi wa daraja,awali eneo hili halikuweza kupitika kirahisi kutokana na kujaa maji,tunawapongeza sana wataalam wetu kutoka Tarura kukamilisha kazi kwa haraka na  kwa viwango”alisema.


Mwajuma Athuman alisema,awali 
akina mama wajawazito waliteseka pindi wanapotaka kwenda kliniki kwani walilazima kuwabeba wajawazito kwenye machela jambo lililopelekea baadhi yao kupoteza maisha kabla ya kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma.


Saidi Mtawanyi,ameiomba 
serikali kuu kuiongezea Tarura fedha za kujenga kipande cha Barabara kilichobaki ili kurahisisha mawasiliano kati ya Kitongoji maarufu cha Zanzibar chenye idadi kubwa ya watu na kijiji cha mama cha Mandepwende.


Alisema,hatua hiyo itasaidia 
kuunganisha mawasiliano ya barabara kati yam kitongoji hicho na maeneo mengine ya wilaya ya Namtumbo ambayo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.


Kwa upande wake meneja wa 
Tarura wilayani Namtumbo Mhandisi Fabian Lugalaba alisema,ujenzi wa daraja hilo umegharimu kiasi cha Sh.milioni 50 na ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 98 na limeanza kupitika.

Alisema,daraja hilo ni sehemu 
ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Lwinga,Mandepwende Msengenengem na ufunguzi wa barabara mpya ya Mfwate hadi Msengenengem yenye  wa kilomita 41  ambayo inayohusisha na ujenzi wa box kalavati 2 ambapo gharama za mradi wote ni Sh.milioni 638.

Alisema,kwa sasa ufunguzi wa 
barabara yote kilomita 41 umekamilika na kazi inayoendelea na ujenzi wa box kalavati mbili na mradi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu ili kuruhusu shughuli na maisha ya wananchi kuendelea kama kawaida.
MWISHO.

Meneja wa Tarura wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mhandisi Fabian Lugalaba akitoa maelekezo kwa  baadhi ya mafundi wanaojenga box kalavati katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Mandepwende- kuelekea kitongoji cha Zanzibar wilayani humo.
Meneja wa Tarura wilayani Namtumbo Mhandisi Fabian Lugalaba akikagua ujenzi wa box kalavati linaloendelea kujengwa katika barabara ya Mandepwende kuelekea kitongoji cha Zanzibar wilayani humo.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Mandepwende-kuelekea kitongoji cha Zanzibar ambacho ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara wilayani Namtumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...