Waziri wa Utamaduni, sanaa na Michezo Balozi Dkt,Pindi Chana ametoa wito kwa vijana (wasanii) wenye vipaji kuendelea kujisajili kupitia baraza la sanaa ili kuendelea kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali.

Waziri amebainisha hayo mkoani Njombe wakati akifungua tamasha la pili la kitaifa la utamaduni linaloendelea kufanyika kwa siku tatu mkoani humo ambapo mikoa yote 31 Tanzania inashiriki katika tamasha hilo.

"Wizara inatoa maokoto,mirabaha ipo vizuri na Rais wetu amekuja na mfuko wa kukopesha watu wa utamaduni kwa hiyo vijana mkajisajiri baraza la sanaa"

Dkt,Pindi Chana amewapongeza watu wa mkoa wa Njombe kwa ukaribisho na kuwapokea wageni kwa kuwa huo ndio utamaduni wa watanzania na sasa wageni wanaendelea kujua vizuri mkoa wa Njombe,hali ya hewa na utamaduni wa vyakula vyao ikiwemo Kande,Numbu na Ulanzi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema tamasha hilo limekuwa na umuhimu mkubwa kwenye kukuza na kulinda utamaduni huku akiwakaribisha wageni na kushugudia utalii wa baridi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...