Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.


KAMPUNI ALAF Tanzania, ambayo ni moja ya makampuni chini ya Safal Group, leo imezindua rasmi dhamana ya bidhaa lengo likiwa ni kulinda ubora wa bidhaa zake kwa wateja.  

Uzinduzi huu unatokana na kutapakaa kwa bidhaa zilizozalishwa chini ya kiwango na na pia bidhaa bandia katika soko la Tanzania na masoko ya nje. 

Meneja Masoko wa ALAF, Isamba Kasaka, amesema dhamana hiyo mpya,inalenga kuwapa walaji amani na kuwahakikishia kuhusu bidhaa za ALAF ambazo ni pamoja na mabati na nondo.

Amesema ALAF imeendelea kushtushwa na wimbi la bidhaa za chini ya kiwango na bidhaa bandia ambazo zinaathiri sekta zote nchini. “Bidhaa hizi pia ni hatari kwa usalama na afa ya walaji,” amesema.

Amesema kupitia program hii ya dhamana hii ya bidhaa wataendelea kutoa elimu kuhusu bidhaa za chini ya kiwango na feki. “Tunafanya kazi kwa karibu na serikali, vyombo vya kuimarisha sheria na vyombo vya uthibiti ili kukabiliana na wimbi hili la bidhaa feki,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Albert Chalamila, ameipongeza lampuni ya ALAF kwa kuibua mjadala huu wa bidhaa bandia. Alitoa wito kwa vyombo vyote vya usimamizi na wadau wengine wote kuimarisha vita dhidi ya wimbi hili. 

Ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kama vile TBS, FCC, OSHA na nyinginezo kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora ili kuwalinda walaji. 

“Walaji wanatakiwa kuichangamkia dhamana hii ya bidhaa ili wajirishishe na ubora wa bidhaa na uhalali wake kabla ya kununua,” alisema na kusiistiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu suala la ubora. 

Kwa mujibu wa Mh. Chalamila, ukosefu wa ubora una athari kubwa za kiafya na usalama kwa walaji na wanatakiwa kulindwa.  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akikata keki mara baada ya  uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na viongozi mbalimbali wakishangilia mara baada ya kuzindua dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza wakati wa  uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...