NA DENIS MLOWE, IRINGA

BARAZA la Wazee la CCM mkoa wa Iringa limelaani vikali na kwa nguvu zote mwenendo uliojitokeza na unaoendelea hivi sasa wa kuigawa nchi katika udini na ukanda juu ya sakata la bandari.

Akitoa tamko Hilo Mwenyekiti wa Baraza Hilo, Amani Mwamwindi alisema kuwa kumekuwa na matamko na maoni mbalimbali kuhusiana na suala la makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai, kuhusiana na suala la Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema kuwa kwa nia njema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fursa kwa wananchi wake kutoa maoni, kuhusiana na suala tajwa hapo juu lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitoa maneno ambayo hayako salama kwa nchi yakiongozwa na udini na ukanda.

"Wapo watu wamechukulia mjadala huu kwa dhamira za kuigawa Nchi kikanda na kidini sisi Wazee wa Mkoa wa Iringa tunakemea kwa nguvu zote tabia hii inayoweza kusababisha kuvunjika kwa Amani, utulivu, umoja na mshikamano wa Nchi yetu ambao tumeurithi kutoka kwa Waasisi wa Nchi hii Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume" Alisema 

Alisema kuwa wanashauri watu watoe maoni kwa lugha ya staha na yenye kujali uzalendo na sio maslahi binafsi.

Aliongeza kuwa Wazee wa Mkoa wa Iringa wapo pamoja na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yake na kumuunga mkono katika uwekezaji mbalimbali unaofanyika kwa maslahi ya Taifa la Tanzania. 

Mwamwindi alisema kuwa Wazee wa Mkoa wa Iringa wanaunga mkono maridhiano ya vyama vya siasa yaliyoanzishwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mustakabali wa Taifa letu, lakini hatukubali wanasiasa kutumia maridhiano hayo kwa kumdhihaki na kumkashfu Mh. Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Daud Yasin alisema kitendo Cha wazee mkoa wa Iringa kutoa tamko la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ni jambo la heri na Kama Chama wako nyuma Yao kwenye tamko lao kwa kuwa wameona mbali suala la baadhi ya watu kutaka kuvunja umoja na mshikamano.

"Chama kimefarijika kuona wazee wanaliunga mkono suala la bandari kwa asilimia mia Moja",Alisema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...