Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa amsema tamasha la Kizimkazi ni miongoni mwa matamasha muhimu kwani limeendelea kuwaunganisha wananchi wote bila kujali itikadi za siasa au dini.

Ametoa kauli hiyo leo kuelekea tamasha la Nane la Kizimkazi baada ya kushuhudia mechi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi Makunduchi visiwani Zanzibar imedhaminiwa na Mwanamke Initiatives Foundation chini ya Mwenyekiti wake Wanu Ameir Hafidh na imemalizila bila kupata mshindi, hivyo itarudiwaAgosti 31,2023.

Akielezea zaidi kuhusu tamasha hilo ambalo linafadhiliwa na kuratibiwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation ambayo Mwenyekiti wake ni Wanu Ameir Hafidh , Waziri Mchengerwa amesema tamasha hilo limekuwa likiwakutanisha wananchi wa maeneo mbalimmbali nchini.

“Wanafika kwenye tamasha hilo bila kujali zao za vyama vya siasa pamoja na itikadi za dini.Hiyo ndio inaleta tafsiri ya Tanzania na hiyo ndio tafsiri ya Zanzibar.

“Kupitia matamasha kama haya watu wanakuwa wamoja, wanashikamana pamoja bila kujali itikadi zao, kwa hiyo matamasha haya ni muhimu kwa vizazi vya leo na kesho,”amesema Waziri Mchengerwa.

Kuhusu mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga , amesema michezo inatukumbusha kuwa na umoja, amani ndio kitu muhimu na wao ambao wako sekta ya utalii wanaamini moja ya jukumu walilonalo ukiondoa vivutio vya asili wanachojivunia nacho ni amani

“Utulivu ni kivutio kikubwa kwa nchi yetu , kwa taifa letu la Tanzania ambalo linatofautiana na mataifa mengi duniani kwasababu amani ukiitafuta utaipata Tanzania.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...