NA K-VIS BLOG, MWANZA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umetwaa tuzo ya mshindi wa pili wa Mashirika, Wakala na Taasisi za Umma kwenye kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki jijini Mwanza (MEATF) 2023.

Maonesho hayo ambayo yamezinduliwa rasmi Agosti 28, 2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe  katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, yameandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), tawi la Mwanza yakilenga kuwaleta pamoja wadau wa masuala ya baishara katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zilizopo.

Sekta ya Viwanda na Biashara ni wadau wakubwa wa WCF kwani waajiri kutoka sekta ya Umma na Binafsi ni wanachama wa Mfuko huo ambao jukumu lake kubwa ni kulipa Fidia kwa mfanyakazi atakayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi alizoajiriwa kwa mujibu wa mkataba.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe (kulia), akimkabidhi kombe na cheti Afisa Matekelezo (Compliance officer) wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Alberto Nyingo, baada ya Mfuko huo kuibuka mshindi wa pili wa Taasisi, Wakala na Taasisiz a Umma (kundi la sekta ya hifadhi ya jamii) katika Maonesho ya18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

Wananchi wakisikiliza maelezo kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye banda la Mfuko, katika maonesho ya18 ya biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Mwanza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...