Na Maelezo.

Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yusuf amekabidhi vifaa vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 27 kwa idara ya katiba na msaada wa kisheria iloyopo chini ya Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora .

Akikabidhi Msaada huo huko Ofisini Kwake Maisara Mjini Zanzibar alisema lengo la msaada huo ni kuwasaidia watoa huduma za kisheria kuweza kutatua matatizo mbali mbali ya kisheria katika jamii sambamba na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Akitolea ufafanuzi wa msaada huo Mkurugenzi huyo amesema kukabidhi vifaa hivyo ni urejeshaji wa huduma kwa jamii na kutekeleza ahadi ya mamlaka hiyo waliyoitoa katika kilele cha siku ya wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika katika Ukumbi Wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni hivi karibuni.

Alieleza kuwa mamlaka imetoa jumla ya Printer kumi na moja,Laptop tano na Vishkwambi viwili kwa wasaidizi wa kisheria wa Wilaya kumi na moja za Unguja na Pemba ili kurahisha kazi zao .

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Hanifa Ramadhan Said ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) kwa kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoa hudua za msaada wa kisheria .

Awali wahudumu hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zililizokua zikirejesha nyuma utendaji wao wa kazi hivyo msaada huo utasaidia kutatua changaoto hizo katika utendaji.

Watoa huduma za msaada wa kisheria ni wafanya kazi wa kujitolea ambao wamekua wakifanya kazi kubwa ya kusaidia jamii kuweza kupata haki zao kisheria.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...