Mratibu wa Mradi Kutoka Shirika hilo Elineca Ndowo (wa tatu kushoto), akikabidhi hundi kwa vikundi vya watu wenye ulemavu katika hafla ya iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za ADD Mikocheni Jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Mradi Kutoka Shirika hilo Elineca Ndowo akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi vya watu wenye ulemavu iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Mnufaika wa Mradi Eva Masanilo (katikati) akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa hundi katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za ADD International, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA: ADD)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM


Katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajengewa uwezo wa kushiriki katika shuguli mbalimbali za ujenzi wa Taifa, Shirika la kuhudumia watu wenye ulemavu nchini ADD International, limezindua kampeni maalum ya kuwawezesha watu hao, ili kuifikia jamii na kuielimisha juu ya haki zao.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Mradi Kutoka katika Shirika hilo Elineca Ndowo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa vikundi vya watu wenye ulemavu iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Amesema Shirika hilo limekutana na watu hao ili kuhakikisha wanajumuishwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo Ajira, Uchumi, Elimu pamoja na Afya, ambapo kulikuwa na mchakato maalum wa kuwapata vijana watakaofanya kazi ya kuifikia jamii, na kutoa elimu juu ya haki za watu wenye ulemavu, ili kuifanya jamii nzima ya Watanzania kuwa na mtazamo chanya kwa makundi hayo.

Hata hivyo Shirika hilo limepata vijana wawili ambao mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Zanzibar watakaoshiriki moja kwa moja katika kampeni za kutetea haki za watu wenye ulemavu.

"Shirika tumebadilisha namna ambayo tunafanya kazi, hapo awali tulikuwa tukifanya kazi za kimaendeleo sisi wenyewe, ambapo tulikuwa tunaenda chini kufanya kazi na watu wenye ulemavu, au taasisi zao. lakini kwa sasa tuna mfumo mpya wa namna ya kufanya kazi" amesema Ndowo, na kuongeza kuwa,

"Taasisi yetu imekuwa ikitoa ruzuku kwaajili ya shughuli za watu wenye ulemavu, na walengwa wa fedha husika wanaingia katika mchakato mzima wa kumtafuta nani apate fedha hiyo" ameongeza.

Amesisitiza kuwa mchakato wa kuwapata vijana hao umezingatia vigezo vilivyohitajika, sambamba na kupitia maandiko yao waliyowasilisha na kisha kuwapata washindi.

Kwa upande wake mmoja wa mnufaika wa Mradi huo, ambaye anaishi na ulemavu wa changamoto ya kuona, Eva Masanilo, amelipongeza Shirika la ADD International kwa kuona umuhimu wa kushiriki kwenye mchakato huo, na hatimaye kuwa miongoni mwa watu waliopata nafasi ya kufanya kazi katika Jamii.

"Jamii yetu bado kuna baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya watu wenye ulemavu, hivyo hii kwangu ni fursa ya kwenda kuwahamasisha na kuwaelimisha kuondokana na mtazamo huo" amesema Masanilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...