NA DENIS MLOWE,IRINGA

MKURUGENZI was Makampuni ya Asas Group, Salim Abri 'Asas' amewataka wamachinga kuwa wamoja kwenye maslahi yao kuliko kwenye mambo ya vurugu Ili waweze kukopesheka.

Akizungumza mara baada ya kuitikia wito wa Shirikisho la Machinga Tanzania (SHIUMA) ambapo alikabidhiwa hati ya pongezi na meza ya biashara na alikubali kuwa mlezi na mwanachama wa shirikisho hilo katika tukio hilo lililofanyika katika soko la Machinga Mlandege mjini Iringa alishukuru wamachinga na kuwapa Somo kuhusu biashara.

Salim Abri Asas ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (MNEC) mkoa wa Iringa alisema kutengeza biashara sio kazi ya lelemama kwani ni jambo linalohitaji uvumilivu, muda na nidhamu kubwa ya fedha.

Asas alisema changamoto kubwa inayowakabili wafanyabishara wadogo ni dhana waliyonayo ya kutengeneza fedha zaidi badala ya kukuza biashara zao katika mlengo wa mbali zaidi katika kuwekeza kwa ajili ya kesho.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara wadogo siku zote wanafikiria faida anayopata kwa kuuza kiwango kile kile cha biashara anayofanya badala ya kuikuza biashara yake na hivyo kumfanya miaka yote kubaki pale pale.

"(Kuna kiongozi Mmoja wa wamachinga alikataa kukuza mtaji wake akisema kwamba akifika hatua ya kuwa mfanyabiashara wa kati cheo chake kitaisha hapo maana ya kwamba hawezi kukuwa kwa kufikiria cheo zaidi kuliko kukuza mtaji wake" alisema

Aidha aliwaahidi wamachinga kufanya makubwa kuliko awali ila matendo na maneno yao ndio yatafanya aweze kufanya makubwa kwao pale ambapo kutakuwa na amani na utulivu na kuondokana na migogoro isiyo na tija.

Alisema atajitahidi kuandaa semina za biashara za mara kwa mara kwa wafanyabiashara hao ili wapate maarifa yatakayokuza biashara zao na kuwafanya katika siku za usoni watoke katika kundi la machinga na kuwa wafanyabiashara wa kati na Kisha wakubwa.

Aliwashukuru kwa viongozi Shiuma Taifa kwa kutumia busara katika kutatua changamoto wamachinga mkoani hapa na kupata viongozi ambao atawapa ushirikiano wa kutosha.Asas ameahidi pia kujenga jengo maalumu kwa ajili ya huduma mbalimbali za watoto ambao mama zao wanaofanyabiashara katika soko hilo ili liweze kuwapatia nafasi watoto kuwa na Eneo la kupumzikia kwenye soko Hilo lililojengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 200 zilizotolewa na yeye mwenyewe.

Awali Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada alisema halmashauri yao inazo Sh Milioni 10 zilizotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya machinga ya wilaya na kwamba mpango wao ni kuongeza fedha na kujenga ofisi kubwa zaidi.

Aidha alisema kwamba halmashauri ya manispaa ya Iringa ilikwishapitisha mkopo wa Sh Milioni 100 kwa ajili ya Saccos ya Machinga wa Mjini Iringa, kinachosubiriwa ili mpate fedha hizo ni ukamilishaji wa uanzishwaji wa Saccos hiyo fedha ziweze kutoka.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanja licha ya kumshukuru Salim Abri kuwa mlezi wa shirikisho Hilo aliendelea kutoa onto kwa onyo kwa uongozi huo akisema atakayebainika kuhamasisha vurugu,maandamano na migomo inayohatarisha amani na usalama wa mali na raia wengine atachukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa jeshi la Polisi kushughulika nao.

Mkurugenzi wa kampuni ya Asas Group Salim Abri 'Asas' akikabidhiwa hati ya pongezi na mwenyekiti wa SHIUMA Matondo Masanja
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas Group Salim Abri akizungumza na wamachinga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...