Njombe
Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi,wamevamia kituo cha mafuta cha Orexy mkoani Njombe usiku wa kuamkia Septemba 3,2023 na kujaribu kuiba, zoezi ambalo halikufanikiwa baada ya polisi kuwasili kwa wakati eneo la tukio na kufanikiwa kuwadhibiti wahalifu hao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa Polisi John Makuri Imori amesema watu hao watatu waliokamatwa baada ya kujeruhiwa na polisi katika majibizano ya risasi,wanahusika na tukio lililotokea siku chache zilizopita la kuvamia nyumbani kwa wakala wa fedha Golden Luoga na kuua watu wawili akiwemo mfanyabiashara huyo pamoja na kaka yake Faraja Luoga.
"Askari waliposhtuka kwamba hawa wanakimbia wakapiga risasi juu ili wasimame na wao wakajibu na walipokuwa wakijibu bahati mbaya na askari wa kwetu nao wakawajeruhi hawa watatu na katika eneo la tukio tumeweza kukamata silaha mbili za moto"amesema Kamanda Makuri
Kamanda Makauri ameongeza kuwa baada ya tukio la mauaji ya wafanyibiashara mkoani humo polisi walijiimarisha kwa kuongeza nguvu kazi kwenye doria za usiku na hatimae siku ya tarehe moja mwezi Septemba walifanikiwa kumnasa mtu moja aliefahamika kwa majina ya Said Mohammed Bakari (52) mkazi wa chamazi Dar es salaam,ambae alikutwa na vitu mbalimbali ambavyo ni mali ya mfanyi biashara alieuliwa katika tukio la uvamizi lililopita.
Aidha kamanda ameeleza kuwa baada ya mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo, alifanikiwa kuwataja wenzie na kisha akaeleeza mipango waliyo nayo ikiwemo kuvamia kituo cha mafuta,mipango iliyowafanya polisi kuweka mtego na kufanikiwa kuwatia mbaroni huku pia wakibaini vitu mbalimbali vilivyokuwa na watuhumiwa hao kuwa ni vya marehemu aliyeuwa kwa risasi hivi karibuni.
"Tumekuta Pos mashine mbili moja ya NMB na beji moja jeusi mali ya Golden Luoga ambaye ni marehemu kwa sasa"alisema Kamanda Makuri
Home
HABARI
Majambazi watatu wajeruhiwa kwa risasi wakipambana na Polisi kituo cha mafuta mkoani Njombe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...