Jeshi la Polisi kupitia
Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu
Septemba 19, 2023 limefanya Semina ya siku moja kwa Maafisa,wakaguzi na
askari wa vyeo mbalimbali wapatao (300) wa Mkoa wa Dodoma na Vikosi katika
ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma kwa lengo la kukumbushana na kujengeana
uwezo kuhusu maswala Kuzuia na kushughlikia vitendo vya ukatili wa kijinsia na
unyanyasaji dhidi ya watoto.
Pia washiriki walikumbushwa maswala ya yahusuyo
Ushilikishwaji wa jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua changamoto
mbalimbali za uhalifu zikiwemo za maadili katika jamii pamoja na kuwahamasisha
maafisa, wakaguzi na askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia Nidhamu,
Haki,Weledi na Uadilifu kwa kujenga taswira njema ya Jeshi la Polisi na
kulifanya Jeshi la hilo kuaminika na Jamii.
Aidha, katika mafunzo hayo Mratibu wa Dawati la
Jinsia na watoto kutoka makao makuu ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman aliwataka askari kujitambua na
kuacha tabia zote za ukatili na udhalilishaji wa Kijinsia katika familia zao na
kuwasisitiza kufuata sheria za nchi hasa katika mahusiano.
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Michezo Makao Makuu ya
Polisi kutoka kamisheni ya Polisi jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Jonas
Mahanga aliwahimiza Polisi kata kutumia michezo katika kuwaunganisha vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...