Na John Walter-Manyara

Serikali imetoa shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Wasichana ya mkoa wa Manyara, inayojengwa katika Kijiji cha Kiongozi kata ya Maisaka wilaya ya Babati.

Akzingumza na wazee, viongozi wa dini na mila mjini Babati katika kikao maalum,mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imetoa fedha za kujenga Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kwamba ujenzi umeanza kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).

 Serikali ilitenga Shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya kujenga shule mpya za Sekondari 1,026 nchi nzima zikiwemo  shule 26 Maalum za wasichana zinazojengwa moja kila mkoa.

 "Katika kipindi alichopo madarakani rais wetu mpendwa Dr Samia Suluhu Hassan katika mkoa wetu pekee ametupatia fedha za maendeleo shilingi bilioni 498" alisema SendigaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...