Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Mlinzi wa Simba SC, raia wa Cameroon, Che Fondoh Malone amepata ajali maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam wakati akitoka uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuwapokea ndugu zake (Kaka zake) ambao wamekuja nchini Tanzania kumsalimia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Ahmed Ally amethibitisha taarifa hizo za kupata ajali Mlinzi huyo, 

Ahmed amesema Che Malone alipata ajali hiyo saa 10 alfajiri kwenye eneo hilo wakati akijaribu kumkwepa Dereva wa Pikipiki (Bodaboda). Gari hiyo iliingia mtarano na kusababisha kupata hitilafu.

“Alikuwa anatoka uwanja wa Ndege kuwapokea ndugu zake waliokuwa wanatoka Yaoundé, Cameroon, lakini taarifa njema hakuna aliyepata majeraha makubwa zaidi ya Kaka yake ambaye alikuwa mbele, alipata majeraha kidogo na kukimbizwa Hospitali kwa matibabu zaidi,” amesema Ahmed Ally.

Vile vile, Ahmed amesema licha ya kuendesha Gari hiyo, Mlinzi Che Malone ahajaumia sehemu yoyote na tayari yupo ‘fit’ kwa ajili ya kujiunga na wenzake kikosini (Simba SC) kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na michezo mbalimbali ambayo inawakabili.

Kwa upande wake, Mratibu wa Klabu (Simba SC), Abbas Selemani amesema Mlinzi huyo alifika uwanja wa Ndege saa 10 alfajiri kuwapokea ndugu zake hao, ambao walikuja nchini Tanzania na Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Airlines.

“Alinipigia simu muda huo kunifahamisha kuwa wamepata ajali, eneo hilo la Mikocheni mkabala na Shule ya Feza, baada ya kugongana na Bodaboda. Tulifika eneo la tukio na tulikamilisha taratibu zote ikiwa kwenda Hospitali na Kituo cha Polisi kwa ajili ya taratibu nyingine, kwa sasa yupo vizuri tu,” amesema Abbas.

Che Fondoh Malone amepata ajili hiyo eneo la Mikocheni wakati akirejea nyumbani kwake Mbezi, Dar es Salaam, kwenye Gari hiyo kulikuwa na watu wanne (4) akiwemo na yeye yaani Kaka zake watatu na yeye.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...