MKUU  wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameongoza wajumbe wa kamati ya Usalama wa Wilaya hiyo kwenye kikao cha kwanza kujadili mapato kutoka taasisi mbalimbali za serikali, ambapo Pamoja na mambo mengine ameagiza kikao hicho kufanyika Kila mwezi.

Akizungumza leo Mgeni amesema  malengo ya kutaka kikao hicho kufanyika kila mwezi ni kuongeza ufuatiliaji kuhakikisha taasisi zote zinafikia malengo kwenye kukusanya mapato pamoja na kutafuta ufunguzi wa haraka inapobainika changamoto inayoweza kukwamisha zoezi hilo.

Amesema kuwawajumbe wa kamati ya usalama watapokea taarifa za makusanyo Kwa Kila taasisi Kujua mwenendo wa makusanyo kila mwezi. 

Amefafanua kuwa taasisi ambazo ni wajumbe wa kikao hicho ni Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mamlaka ya mapato nchini (TRA), Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Mamlaka ya usimamizi wa wanyama Pori  nchini (TAWA). Wakala wa kudumu za Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira vijijini  RUWASA.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...