--Utekelezaji wafikia 96%

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji Butimba unakwenda vizuri na kasi inaridhisha.

Amesema hayo leo 12.09.2023 katika ziara yake na Kamati ya Usalama Wilaya Nyamagana kwenye mradi wa Maji Butimba akiwa ameambatana na Menejimenti ya MWAUWASA ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Neli Msuya.

Ziara hiyo imelenga kujionea maendeleo ya mradi kuelekea siku ya majaribio ya awali ya mradi huo Septemba 15, 2023.

"Niwapongeze MWAUWASA kwa kazi nzuri na kasi hii ya utekelezaji mnayoendelea nayo, niipongeze pia timu iliyoundwa na Mhe. Jumaa Aweso, Waziri wa Maji kwa ushirikiano huu mnaoutoa kwa MWAUWASA, tuna imani tutapata matokeo chanya," amesema Mhe. Makilagi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Ndg. Neli Msuya amesema utekelezaji wa mradi sasa umefikia asilimia 96 na kuongeza kuwa majaribio ya mradi yatakayoanza tarehe 15 Mwezi Septemba ni hatua ya awali kuelekea katika hatua ya ukamilishwaji.

"Tunakwenda kwa awamu, majaribio haya yatatupa matokeo chanya katika upatikanaji wa huduma ya Maji kwa awamu. Wananchi wataanza kuona mabadiliko kadri siku zinavyokwenda. amesema Ndg. Neli.

Mradi wa Maji Butimba unatekelezwa kwa gharama ya Tsh. Bilioni 69 na utazalisha kiasi cha lita milioni 48 kwa siku na utahudumia zaidi ya wakazi 450,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...