Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MADUKA ya Haier/GSM na Azam TV wameingia ushirikiano wa kibiashara ambapo sasa bidhaa pacha itapatikana rasmi katika vituo mbalimbali vya Azam hasa luninga ya Haier 32 “HD iliyounganishwa na Kisimbuzi cha Antena kwa bei nafuu sambamba na kifurushi cha Sh.25000.
Akizungumza leo Septemba 21,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Meneja Mauzo Azam TV Tanzania Adam Ndimbo amesema ushirikiano huo unakwenda kujibu maswali ya muda mrefu ya wapi kitapatikana kisimbuzi cha bei nafuu pamoja na luninga.
“Ushirikiano huu umejibu maswali hayo sasa kwa kuunganisha huduma bora ya kisimbuzi na Tv bora .Hii imewezekana kupitia kampeni yetu ya burudani mwamwi yaani Mwanzo-Mwisho-Mzigo wa kibabe,”amesema Ndimbo.
Ameongeza luninga hiyo Haier 32“ iliyounganishwa na Kisimbuzi cha Antena inapatikana kwa bei ya wote , nafuu na kawaida ya thamani ya Sh,359000 ikiwa na zawadi ya kifurishi cha Sh.25000 huku akifafanua kwa sasa luninga hiyo inapatikana katika maduka yote ya Haier Tv jijini Dar es Salaam pamoja na Migodi/maduka ya Azam TV.
Akieleza zaidi amesema uzinduzi huo utatingisha katika maeno mbalimbali yakiwemo ya Kanda ya Ziwa,Kaskazini,Kati, Kusini na mikoa yote huku akieleza wananchi wote wa Tanzania wamepewa nafasi sasa ya kumiliki Tv bora ya Haier iliyounganishwa na Kisimbuzi cha Azam bila mawaa kupitia maeneo na maduka hayo.
Kwa upande wake Ibrahim Kiongozi kutoka Haier amesema ushirikiano huo unaashiria hatua muhimu kwa kampuni zote mbili katika kurahisisha utoaji burudani nchini.
“Teknolojia ya hali ya juu ya Haier katika vifaa vya nyumbani pamoja na utalaam wa Azam TV katika utoaji wa burudani za kidigitali vitaleta tija kwa wateja na wasambazaji wa bidhaa hizo zote mbili.”
Ameongeza kuwa bidhaa hizo zinapatikana Tanzania nzima kuanzia mikoa ya Dar es Salaam , Kanda ya Kati ,Kanda ya Ziwa , Kanda Kaskazini na Kanda ya Kusini.
Ibrahim Kiongozi (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Azam TV na Hair Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalibali wa masuala ya burudani na biashara.
Meneja Mauzo wa Azam TV Tanzania Adam Ndimbo(wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Azam TV Tanzania Ltd na Haier Tanzania uliofanyika leo Septemba 21,2023 jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...