Na Mwandishiwetu, Michuzi TV 


Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umedhamiria kutoa huduma iliyo bora katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kutumia watumishi wenye welendi, ari na Teknolojia inayofaa.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba katika mkutano na wahariri wa vyombo vya Habari uliobeba kauli mbiu ya 'Mageuzi yenye tija kwenye Taasisi za Umma kwa maendeleo ya Taifa '

"Dhima yetu ni kutoa huduma iliyo bora katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kutumia watumishi wenye welendi, ari ya kazi na teknolojia inayofaa ili kuhakikisha huduma kwa wanachama wetu inakwenda vizuri.

Majukumu makuu ya mfuko huu ni kama ambavyo yalikuwa kwenye mifuko hiyo mingine kabla ya kuungana. La kwanza ni kusajili wanachama na hii ipo kwa mujibu wa wa sheria, mfuko huu wa hifadhi ya jamii unashughulika moja kwa moja na watumishi wa umma na ule unaohusika na wa sekta binafsi. Sisi PSSSF tunashughulika na na mfuko wa Umma. Amesema na kuongeza kuwa.

Jambo lingine ni kuanisha mafao yanayotolewa na hiyo mifuko. Mifuko hii ilikuwa inashighulika na kuwahudumia wanachama wanazotoka kwenye eneo moja la kazi au ajira katika nchi hii moja kila mfuko unatoa mafao tofauti tofauti, hii nayo ilionyesha iko haja ya kunganganisha mifuko hii itoe mafao yanayolingana.

"Tunakusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama na ni toka mwanachama anaposajiliwa mpaka atakapostaafu nankuingia upande mwingine wa kulipwa mafao, lakini tuapokusanya michango hii mingine baada ya kulipa inayobaki tunawekeza na kulipa mafao.

Aidha amesema katika kipindi cha miaka mitano wamekusanya zaidi ya tsh tilioni 9 huku tsh tilioni 2.17 yamakusanyiko hayo ni deni lililolipwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya deni la tsh tilioni 4.6.

Huku katika sekta ya uwekezaji amesema PSSSF imewekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo majengo, hisa na sekta mbalimbali kama viwanda, huku kwenye majengo ni asilimia 15 tu ya uwekezaji mkubwa walioufanya,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Serikali yake kulipa sehemu ya deni la tsh tilioni 4.6, kwa maana ya tsh tilioni 2.17 zilizolipwa.

"Tushiriki kumshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kulipa hili deni la tsh tilioni 2.17 kati ya tsh tilioni 4.6 zinazodaiwa. Mifuko imeungana na sasa tunaweza kuona kazi iliyobora. Waandishi wa habari tunapoandika mambo hatuna nia ya kumchimba mtu, tunazungumza na wataalamu, tunaangalia historia, baadae tunaona kwba muelekeo uliopo jambo fulani lisipo fanyika pamoja na urafiki tulionao tunaweza tukajikuta nchi inapoteza.

"Mheshimiwa Rais kulipa hizi tsh tilioni 2.17 kati ya tsh tilioni 4.6 deni lililoshindikana miaka 20 ni wazi kwamba hata uwasi wenu umeongezeka. Lakini pia umedadavua vizuri kwamba ukwasi wenu ukiongezeka watu wanaokopa kupitia benki nao tayari wanakuwa wanapata mikopo bila kusubiri ile presha ya Dola.

Kwa pamoja tushirikiane kuwapongeza (PSSSF), hatuwapongezi kwa mafanikio waliyoyapata, lakini pia niwakumbushe PSSSF amekuwa mdau mkubwa wa tasnia ya habari kwa kitudhamini katika shughuli zetu mbalimbali". Amesema Mkurugenzi wa Jukwaa la wahariri TEF Deodatus Balile.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...