MSANII wa muziki wa injili Jesca Honore amewaomba Jamii kujitokeza katika kongamano la Injili litakaloenda sambamba na upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza chini madaktari kutoka Texas , Marekani.

Akizungumza na Michuziblog Honore amesema kongamano hilo litahudumiwa na mhubiri wa Kimataifa na daktari Rod Dennis na jopo la madaktari wengine kutoka nchini Marekani kwa kushirikiana na madaktari wa hapa nchini.

"Kwenye mkutano huu wa nguvu ya kuinua mataifa, kutakuwa na uponyaji wa kiroho na kimwili, nitakuwa na waimbaji wengine kuwaburudisha na watu kuguswa na Mungu kwa njia ya uimbaji, kwa hiyo watu wasikose huduma hizi bure."

Kwa upande wake, mmoja wa waratibu Emanuel Ezekiel ameeleza kongamano hilo litafanyika viwanja vya TTCL Kijitonyama Dar es Salaam kuanzia Septemba 20 na 21,2023 na kuwahimiza watu wa madhehebu yote wajitokeze kwa wingi ili wapate kupima.

Mratibu wa huduma hiyo Ben Christopher kutoka Finland amewataja wasanii wengine watakaokuwepo ni Agape gospel singers, Rehema Simfukwe, Emmy Charles, Masi Masilia, John Kavishe na Harun Laston 'Zoravo'.

Mchungaji wa Kingdom of Embassy Fred Kimiti amefunguka kuwa watu wengi wamekaa wakitegemea roho wa Mungu atashuka na kuwaponya jambo ambalo sio, kwani watu wanatakiwa wapime afya zao ili kujitambua mapema na kuchukua hatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...