DAR ES SALAAM 15 SEPTEMBA 2023

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema Jeshi hilo limewekeza Zaidi katika kufanya utafiti, elimu na mafunzo ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa jamii.

IGP Wambura amesema hayo wakati aliposhirikia hafla ya utiaji Saini Hati ya mMkubaliano na Mashirikiano baina ya Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Chuo cha Taluma ya Polisi Dar es salaam ambapo ushirikiano huo utawesha Jeshi hilo hasa eneo la mafunzo na tafiti mbalimbali.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo amesema kuwa, Jeshi la Polisi litaendekea kufaidi mashirikiano yaliyopo na Chuo cha Uhasibu Tanzania ambapo changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii zitapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es salaam Dkt. Lazaro Mambosasa amesema kuwa, mashirikiano kati ya Jeshi la Polisi kupitia Chuo cha Taaluma  na Chuo cha Uhasibu Tanzania ni ya awali ambayo yamejikita zaidi hususani kwenye eneo la usalama.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...