jumla ya sh milioni 749 zinatumika kujenga shule mpya sekondari ya Mkungo iliyopo Chato mkoani Geita ikiwa ni miongoni mwa moja ya miradi mingi inayoendelea kufanywa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf mkoa wa Geita ambayo itarahisishia watoto kutembea umbali mdogo kufata elimu.
Mradi huo ambao utafanikisha ujenzi wa jengo la utawala, nyumba za walimu 2, kisima cha maji, matundu 28 ya vyoo pamoja na maktaba utasaidia maendeleo makubwa ya elimu katika kijiji cha Mkungo.
Akitembelea mradi huo Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala bora George Simbachawene aliwapongeza TASAF kwa kufanikisha mradi huo ambapo mpaka sasa pesa iliyotumika ni ndogo ukilinganisha na ubora wa majengo unavyoonekana.
Aidha alimpongeza mbunge wa Chato Medard Kalemani kwa kufanikicha maendeleo ya katika jimbo hilo hasa katika sekta ya elimu ambapo katika kipindi cha miaka mitatu zimejengwa shule 19.
Simbachawene aliongeza kuwa shule hii itawasaidia watoto kupata elimu kwa urahisi zaidi ambapo mwanzo iliwalazimu kutembea umbali mrefu kufata shule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...