Mji Mkongwe Zanzibar, Tanzania na Geneva, Uswisi, Septemba 15, 2023

Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited imeungana na kampuni ya TP Company Limited ya Zanzibar, ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies (Vigor Group), ili kuimarisha ugavi na usambazaji wa gesi ya LPG (liquefied petroleum gas) katika visiwa hivyo.

Hatua hiyo inafuatia uundwaji wa kituo cha kwanza cha gesi ya LPG visiwani, Ikiwa ni sehemu ya dhamira pana ya Oryx Energies Group kutimiza ajenda ya mpito ya nishati, ambayo inahusisha kuhakikisha upatikanaji wa gesi hiyo kwa masoko ya Afrika na hasa kwa Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar.

Katika makubaliano yenye sehemu mbili, TP Company Limited ikisaidiwa na Oryx Energies inajenga kituo cha kwanza kabisa cha LPG Zanzibar, chenye uwezo wa MT 1,300. Kituo hicho kinatarajiwa kukamilika katika robo ya nne ya mwaka 2023, kituo hiki kipya kitaendeshwa na kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited pekee kwa muda mrefu, na hivyo kuhakikisha ubia wa kudumu.

Wakati huo huo, Oryx Gas Zanzibar Limited itakuwa inanunua 100% ya mali za biashara ya LPG za TP Company Limited, ambazo kwa sasa zinatambulishwa na kuendeshwa kwa jina la VGas. Mali hizi zitabadilishwa na kuwa chini ya jina la Oryx Energies hatua kwa hatua. Kwa upande wake, TP Company Limited inachukua asilimia 30 ya hisa za Oryx Gas Zanzibar Limited. Makubaliano haya yatakuwa na sifa za kipekee, yakiweka mwanga kwa dhamira ya Oryx Energies kama kampuni kusaida mipango ya jamii na kukuza ushirikiano wa ndani.

Ikiwa kampuni ya uendeshaji wa kituo kipya cha LPG, Oryx Gas Zanzibar Limited itawasambazia gesi wateja wengine pia, na hivyo kusaidia kuhakikisha upatikanaji wa gesi ya uhakika, endelevu na usio na vikwazo kwa wakazi wa Zanzibar. 

Hatua hiyo pia inashughulikia hali ngumu ya kihistoria ya usambazaji wa ndani wa gesi ya kupikia, ambapo taratibu nyingi za uendeshaji na usimamizi zimeongeza gharama kwa Wazanzibari na mara nyingi kusababisha vikwazo.

Shuwekha Khamis, Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Limited, alisema: “Maendeleo haya ya ushirikiano na kampuni kubwa ya ndani ya nchi yanahakikisha dhamira yetu kuwapatia wakazi wa eneo hili nishati safi ya kupikia. LPG ina nafasi kubwa katika mchanganyiko wa nishati Zanzibar, na inahakikisha usalama wa nishati muhimu ya kupikia na pia kusaidia maendeleo ya sekta ya utalii wa ndani.”

Benoit Araman, Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Limited, aliongeza: “Kwa muda mrefu tumekuwa tukijenga misingi ya upanuzi huu, baada ya kufikisha LPG katika visiwa vya Zanzibar tangu mwaka 2010, ushirikiano huu ni hatua muhimu ya kuimarisha zaidi usambazaji wa gesi ya LPG Zanzibar.”

Abdallah Salim Turky, Mkurugenzi Mtendaji wa Vigor Group, alisema: "Kuundwa kwa kituo kipya cha LPG kunaendana kikamilifu na maono yetu ya kuwa mstari wa mbele katika kutoa bidhaa na huduma za hali ya juu ndani ya nchi kutoka kwa masoko ya kimataifa kufikia jamii yetu kwa bei wanazoweza kumudu. 

Hii itasaidia kuboresha viwango vya afya na ustawi wa Zanzibar na pia itasaidia kulinda mazingira kwa kutoa njia mbadala, salama na ya uhakika kwa matumizi ya mkaa na kuni.” Aliongeza: “Ili kufanikisha hili, tunayofuraha kuingia ubia na Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited, Kampuni na timu nzima imejijengea sifa na umaarufu kama mshiriki anayetambulika vyema kwenye soko la reja reja.

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Limited, Benoit Araman akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Unguja Zanzibar wakati kutangaza kuungana kwa makumpuni ya gesi ya Oryx Gas Zanzibar Limited na TP Company Limited ya Zanzibar ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies ili kuwezesha wakaazi wa Zanzibar kupata nishati safi ya LPG kwa gharama nafuu


Mkurugenzi Mtendaji wa Vigor Group, Abdallah Salim Turky akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Unguja Zanzibar wakati kutangaza kuungana kwa makumpuni ya gesi ya Oryx Gas Zanzibar Limited na TP Company Limited ya Zanzibar ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies ili kuwezesha wakaazi wa Zanzibar kupata nishati safi ya LPG kwa gharama nafuu

Mtendaji mkuu ORYX ENERGIES ZANZIBAR Shuwekha Muhamed Khamis


Kutoka kushoto kwenda kulia: Toufiq Salim Turky (Mwenyekiti wa Vigor Group), Benoit Araman (Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Limited), Shuwekha Omar Khamis (Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Limited), Abdalla Salim Turky (CEO wa Vigor Group).





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...