KAMPUNI ya Dough Works Limited, wamiliki wa KFC Tanzania wamesherehekea hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu ilipofungua biashara yake kwa wateja nchini kwa mara ya kwanza Mei 2013.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Mgahawa wa KFC Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023, Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai, amesema mafanikio ya chapa hiyo yanazingatia ubora wa uendeshaji.

“Chapa ya KFC inaendeshwa na watu wanaohudumia, wafanyakazi wetu, watu tunaowahudumia wateja, na wale wanaochangia ukuaji wa chapa hii, wamiliki nyumba, wadhibiti ubora, washauri na washirika mbalimbali tunaofanya nao kazi, tungependa kusema, asante kwa miaka 10 ya kupata huduma ya chakula kizuri nchini Tanzania.

Tunapoingia katika enzi mpya ya KFC, tunaahidi kuendelea kuhudumia na kutoa huduma ya chakula hususani kuku wa kukaanga watamu zaidi kwa njia mpya za kibunifu, kufanya kazi nao na kupata kutoka kwa wachuuzi wa ndani, na kuendeleza huduma za kipekee kwa wateja wetu.”

Desai amesema kuwa KFC imetoa ajira ya moja kwa moja kwa zaidi ya wafanyakazi 250 na imesaidia mamia ya familia na jamii kwa ujumla.

Wakiwa katika sherehe hizo, KFC imekumbushia uwepo wa mgahawa wa Mikocheni ambao umeshuhudia uwepo wa wateja wengi ambao wamekuwa wakipanga foleni kupata huduma ya chakula kabla hata milango haijafunguliwa, ikihudumia wateja karibia 1,000 katika siku yake ya kwanza ya biashara nchini, Tanzania.

Amesema Katika kusherehekea miaka 10 ya KFC- Tanzania pia imezindua kampeni yao ya Kusherehekea Miaka 10, ikitoa ofa tatu (3) mpya za milo zinazotolewa pamoja na chipsi na soda kwa TZS 16,000 zinapatikana kwa muda mfupi tu hadi Novemba14, 2023.

Kwa Upande wa Mfanyakazi wa KFC-Tanzania Shafii Idege uwepo wa chakula kitamu na kupunguza gharama kwa bidhaa za KFC, wateja 1,000 waliobahatika zaidi watapata fursa ya kualikwa kwenye chakula kitakachoandaliwa kwa ajili kushereheka uwepo wa KFC na kupata vyakula na burudani.

Kwa Upande wa Mfanyakazi wa KFC tangu inaanzishwa, Christina Nzegera amesema amemshukuru Mungu wa Kumuweka kuwa Mfanyakazi Tangu inapoanzisha na sasa inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa hapa nchini. 

"Kujitoa, Kujituma, na kujikomiti katika kazi nilianza kama mfanyakazi wa kawaida hadi sasa tunasheherekea miaka 10 pamoja, nimepata marafiki wengi.....hadi sasa nimekuwa meneja wa wa moja wa migahawa ya KFC Tanzania." Amesma Christina

Pia ametoa wito kwa vijana wasikubali kuridhika mahali walipo kwa sababu kinachofanya mtu asifike mbali kwa sababu wanaridhika na pale walipo na hawafanyi kazi ili kuwa bora zaidi.

Pia amesema KFC -Tanzania inatoa nafasi ya kujifunza, amekuwa na ujuzi ambao umeweza kubadilisha maisha yake na amepata ujuzi ambao mtu hawezi kuung'oa Kichwani kwake.

Kwa upande  wa Mteja wa KFC, Mnzelu Malongo amesema kuwa anafurahia huduma za KFC kwa sababu wana huduma kwa wateja nzuri kwa wateja pia wanaukarimu kwa wanunuzi wa vyakula katika migahawa yao.
Wafanyakazi wa KFC wakikata keki ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 10 tangu ianzishwe hapa nchini. Keki hiyo ikmekatwa leo Septemba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai, akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023 wakati wa kusheherekea miaka 10 ya KFC-Tanzania tangu kuanzishwa kwake apa nchini.
Upande wa Mfanyakazi wa KFC-Tanzania Shafii Idege akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023 wakati wa kusheherekea miaka 10 ya KFC-Tanzania tangu kuanzishwa kwake apa nchini.
Mteja wa KFC, Mnzelu Malongo akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2023 wakati wa kusheherekea miaka 10 ya KFC-Tanzania tangu kuanzishwa kwake apa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...