Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo.

Pia amepata maelezo kuhusu huduma za uchunguzi na elimu ya saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa GGML ambapo hadi jana zaidi watu 1000 wamefanyiwa vipimo.

Akitoa maelezo kwa Makamu Rais huyo wa Zanzibar ambaye ndiye mgeni rasmi anayefunga maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku 10, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia amesema kampuni hiyo ndio inayoongoza kwa kuwa muajiri bora nchini.

Pia inaongoza kuwa kuzingatia sheria ya local content Pamoja na kuzingatia masuala ya usalama kazini.

Pamoja na mambo mengine amesema GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amemshukuru Makamu huyo wa Rais kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.
Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia zawadi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.
Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia maelezo  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman kuhusu shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya madini. Makamu huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...