Na Byarugaba Innocent, Kibaha.

Taasisi ya Miriam Odemba 'Miriam Odemba Foundation' yenye makao yake Jijini Dar-eS-Salaam inatarajia kujenga matundu zaidi ya 40 kwenye shule ya Msingi Mwendapole pamoja na kukarabati jengo chakavu linalosomewa na watoto wa Elimu ya awali ili kuwafanya wanafunzi kufurahia masomo yao

Hayo yameelezwa na msemaji wa taasisi kwa niaba ya Miriam Odemba alipofika kuitembelea shule hiyo kupata taswira halisi ya uhitaji na gharama zake akiambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mussa Ndomba

Akiwasilisha taarifa ya uhitaji, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ndugu  Rajabu Chalamila amesema kuwa jumla ya wanafunzi waliopo ni 1004 wanaotumia matundu matatu tu wakiwemo watoto 90 wa Elimu ya awali (chekechea)

Aidha, ndugu Chalamila ameongeza kuwa katika hali ya Kawaida, Shule ilipaswa kuwa na matundu 46 lakini wanapungukiwa na 43 kwani yaliyopo ni matundu matatu tu hivyo nguvu ya haraka inahitajika ili kuwanusuru watoto hao hasa wa kike dhidi ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo UTI.

"Nawashuru Sana wazazi.Tuliwafuata kuwaomba wameweza kuchangia na kujenga matundu 10 ili kuwawezesha watoto kujisitiri, hata hivyo hayajakamilika na kufanya tatizo kuendelea kuwepo" amesema Chalamila

Akizungumzia upande Walimu, Chalamila amebainisha kuwa nako Kuna changamoto kwani walimu wa kike wapo 21 lakini wanatumia matundu 2 ya Vyoo na kuhatarisha afya zao

Mwakilishi wa Miriam Odemba Foundation ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwaruhusu kufanya kazi ndani ya Halmashauri ya Mji Kibaha na kwamba wameona uhitaji, wamechukua picha na wataziwasilisha kwa Miriam Odemba ambaye kwa Sasa yupo nchini Ufaransa akiendelea na shughuli zake za uanamitindo

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwendapole Ndg. Muhidin Mohamed ametoa salaam za Mtaa na kuipongeza taasisi ya Miriam Odemba  kwa kuamua kuanza na Shule ya Msingi Mwendapole. Aidha, ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha muda wowote ule watakaouhitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...