Waziri wa nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na watu wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako,akifungua  mafunzo maalum ya OSHA Jijini Arusha ya kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti kuhusu maduala ya Afya na usalama mahali pa kazi.
Hadija Mwenda ni  mtendaji mkuu wa OSHA Akifafanua juu ya mada mbalimbali zitakazoongelewa katika mafunzo hayo Maalum Jijini Arusha. 
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti, Daniel Sillo alishukuru kwa kamati h kupata mafunzo hayo ikiwa ni matokeo ya kikao chao na Osha kilichoketi mkoani Dodoma na kuahidi kuisaidia Osha 
Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuuu kazi ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja 
Na Vero Ignatus,Arusha

Wakala wa usalama na Afya Mahala pa Kazi,(OSHA) wametakiwa kuendelea  kukagua maeneo ya kazi na kufanya uchunguzi wa afya za wafanyakazi,na kutoa mafunzo ya namna ya kudhibiti madhara ya vihatarishi, ili kulinda nguvu kazi ya taifa, uwekezaji pamoja na kuepuka kuwa sehemu ya kuzalisha wagonjwa na wenye ulemavu bali patumike kukuza uwekezaji. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na watu wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako Jijini Arusha  Ndalichako,wakati akifungua mafunzo maalumu ya Osha kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti kuhusu maduala ya Afya na usalama mahali pa kazi.

Prof. Ndalichako alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kukua kwa uchumi ulimwengu unakabiliwa na viatarishi vingi mahai pa kazi,hivyo ameitaka Osha kuja na mbinu moya ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kazini pamoja na kutoa elimu endelevu kwa wafanyakazi

"Masuala ya usalama na afya ni masuala mtambuka na yanagusa sekta zote za uchumi na tutambue kuwa ulimwengu wa kazi unakabiliwa na vihatarishi vingi vitokanavyo na ukuaji wa uchumi, mabadiliko ya teknolojia na ushindani wa kibiashara haya yote yanahitaji mbinu 
mpya au mbadala kuweza kubaini na kudhibiti athari ya vihatarishi hivyo".alisema

Prof. Ndalichako alisema kwamba mafunzo haya ni utekelezaji wa maagizo yako uliyoyatoa tarehe 24 Agosti 2023 Kamati  ilipokutana na Watendaji wa OSHA kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na. 5 ya mwaka 2003,hivyo Katika majumuisho kamati ilielekeza OSHA kuandaa mafunzo rasmi na ziara kwa Wajumbe wa Kamati kwa lengo la kujifunza na kufahamu vizuri majukumu ya OSHA.

"Nimetaarifiwa pia kuwa kutakuwa na ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kazi kujionea namna ambavyo maeneo hayo yanatekeleza sheria na nmna ambavyo huduma za OSHA zimewezesha kukua kwa biashara zao na kuongeza thamani ya bidhaa zao, ni matumaini yangu pia baada ya mafunzo na ziara hizi kamati yako itakuwa na uelewa mpana kuhusu umuhimu wa masuala ya usalama 
na afya kwa wafanyakazi na hivyo kuishauri vyema serikali" Alisema

Kwa upande wake Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuuu kazi ajira na wenye ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kuwa watu zaidi ya 6400 hupoteza maisha kila siku duniani kutokana na magonjwa na ajali zitokanazo na kazi. 

''Hali ya ajali na gharama za fidia ni kubwa kwa Taifa mwajiri najamii kwa ujumla, hivyo kuna haja ya kuhakikisha madhila vinapunguzwa kwa kila mwajiri kwa kusimika mifumo ya Afya na Usalama mahali pa kazi"alisema

Luhemeja alisema kuna baadhi ya mifuko ya jamii hapa nchini  kwa kipindi cha mwaka. 2020-21ajali zilizoripotiwa zilikuwa 1859 vifo 75 sabamba na hayo gharama za fidia zimeongezeka kutoka bil. 13.19 kwa kioindi kinachoishia juni 2022 na kufikia bil.17.9 kwa kipindi kinachoishia juni 2023

Hadija Mwenda ni  mtendaji mkuu wa OSHA ameelezea  lengo la kuendesha  mafunzo hayo kuwa mpango mkakati wa kuongeza uelewa kwa wadau mbalibali ikiwemo kwa kamati ya Bunge ya Bajeti ambao ndio watunga sera na ndio wanaopitisha bajeti ya serikali waweze kuwa na uelewa wa kutekeleza majukumu yao na kuishauri serikali.

"Majukumu yetu sisi kama OSHA ni pamoja na kulinda uwekezaji na kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi unakuwa na kuimarika na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji na. Kihakikisha wanakuwa salama kazini. 

Bi Mwenda aliishukuru serikali kuendelea kuiamini hata  kuwapatia vifaa vya kisasa vyenye thamani ya sh bilioni 4.3 pamoja na magari 13 waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi haswa kuzingatia Afya na Usalama mahali pa kazi

Aidha takwimu za shirika la kazi duniani zinaonyesha kwa mwaka takrinani wafanyakazi 2,300,000 wanakufa kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, kati ya hizo vifo vya ajali ni 350,000 magonjwa yanakadiriwa kuwa 1,950,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Back To Top