Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Auckland New Zealand.

Mkutano wa 60 Jumuiya ya Polisi wa kike duniani IAWP Umefungwa rasmi siku ya jana septemba, 2023 hapa New Zealand Auckland.

Katika ufungaji huo wajumbe walishukuru kwa namna ambavyo Mkutano huo umewajenga kifkra na kuwaongezea maarifa mapya ambayo yataongeza chachu ya kiutendaji kutokana na mada mbalimbali zilizofundishwa katika Mkutano huo wa sitini.

Aidha wajumbe walipata fulsa ya kuonyesha Utamaduni zao ikiwa ni sehemu ya kutangaza tamaduni za kila nchi na kuonyesha tamaduni hizo Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi sitini na tano kutoka bara la Ulaya na Afrika.

Ambapo Kamishna wa Polisi Utawala na rasilimali watu CP Suzan Kaganda amewaomba wajumbe wa IAWP kufika Nchini Tanzania kushuhudia vivutio vya utalii na tamaduni pamoja na mali kale zilizopo Tanzania bara na Zanzibar huku akibanisha kuwa anaamini watafurahi kuona namna Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na vivutio ambavyo havipo nchi nyingine duniani kama vile fuvu la binadamu wa kwanza olduvai George katika bonde Kreta ya Ngorongoro.

New Zealand wamekabidhi Majukumu yote kwa Mkutano kwa ajili ya Mkutano ujao wa 61  IAWP, 2024 unaotegemea kufanyika Nchini Marekani jimbo la Chicago.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...