Ubalozi wa Uswizi Nchini kwa kushirikiana na Mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji Mkoa wa Morogoro MVIWAMORO wameandaa bonaza la kutekeleza maendeleo ya ujuzi kwa vijana zaidi ya 1600 kutoka Wilaya tano za Mkoa wa Morogoro lengo likiwa ni kuongeza uelewa wa dhana ya ukuzaji wa ujuzi wa ufundi.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Morogoro Afisa Programu wa Kitaifa, Ubalozi wa Uswizi Rasheed Mbalamula amesema Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania kupitia mradi wa fursa za ajira kwa vijana OYE na Mradi wa Ujuzi kwa ajira SET umewekeza fedha nyingi katika kujenga ujuzi wa elimu ya ufundi stadi kwa vijana wa kitanzania hasa katika sekta ya Kilimo kwa zaidi ya miAka mitano.

Bonaza hilo litafanyika katika Wilaya za Kilombero, Mvomero, Ulanga, Gairo na Kilosa ikiwa ni muendelezo wa mradi SET unaotekelezwa na Swisscontact na OYE unaotekelezwa na SNV na kufadhiliwa  na Uswizi.

`

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...