Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imefanikiwa kuibuka mshindi wa Tuzo ya Kampuni Bora ya Kimataifa ya Mwaka iliyotolewa  na waandaaji wa Kongamano la Nishati Tanzania 2023.

Akizungumza wakati akitangaza tuzo hiyo , Muandaaji wa Kongamano hilo la kimataifa, Abdulsamad Abdulrahim amesema Oryx Energies ndio mara yake ya kwanza kupata tuzo hiyo ya kampuni ya kimataifa katika sekta ya nishati.

Ameongeza ni tuzo ambayo imejitokeza katika kipindi cha miezi 12 iliyopita na kuchangia kibiashara na kiufundi katika kukuza sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania.

Abdulrahim mefafanua tuzo hiyo pia inalenga kutambua uvumbuzi na Ubunifu kupitia biashara na ubunifu pamoja na kufanya mabadiliko mazuri katika sekta hiyo.

"Tuzo hii ni maalum kwa kampuni au Shirika ambalo lilitoa mchango bora kwa tasnia nchini Tanzania na kujidhihirisha kuwa kiongozi wa tasnia katika nyanja yoyote maalum ya sekta ya thamani ya mafuta na gesi.

" Kupitia maendeleo ya watu, kampuni ambalo lilipanua maarifa na kujifunza katika nyanja za kibiashara au kiufundi za sekta ya mafuta na gesi, "amesema Abdulrahim alipokuwa akielezea tuzo hiyo.

Akieleza zaidi amesem katika kutafuta mshindi, kura zilipigwa kupitia ukurasa wa Tanzania Energy Congress 2023 na Oryx Energies kuibuka kinara kwa mwaka huu 2023."Hongera timu ya Oryx kwa mchango wa ajabu na mawazo ya ubunifu ili kuharakisha ukuaji wa sekta ya LPG nchini Tanzania."

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite Araman akizungumza kwa niaba ya timu nzima  Oryx baada ya kupokea tuzo hiyo amesema Oryx Gas imefanya mengi sana kwa jamii kwa kipindi kifupi sana.

Ametoa mfano Oryx Gas  imetoa mitungi na majiko  zaidi ya 13,000 kwa wanawake toka makundi mbalimbali nchini Tanzania katika muendelezo ule ule wa Nishati safi ya kupikia kwa wote.

Ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan  kupitia REA kwa kutoa ruzuku kubwa kwa mitungi ya gesi kwa wananchi.Muandaaji wa Kongamano la Kimataifa la Nishati Tanzania mwaka 2023 Abdusamad Abdulrahim (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Kampuni bora ya Kimataifa ya mwaka 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite Araman( kushoto)wakati wa kongamano  hilo linalofanyika jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...