NA K-VIS BLOG, GEITA.
WANACHAMA
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kutumia
fursa ya Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya
Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje (EPZA) mkoani
humo Geita, kufika kwenye banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa na kupata elimu
inayohusiana na uanachama wao, Meneja wa
PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Geofrey
Kolongo, amesema.
Ameyasema
hayo leo Septemba 22, 2023 kwenye banda la PSSSF, kwenye maonesho hayo ambayo PSSSF
ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki ili kuwahudumia wananchi na
watumishi wanaoshiriki katika maonesho hayo.
“Tunatoa
huduma zote ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini, ambambo
mwanachama ataweza kupata taarifa za Michango yake, taarifaz a Mafao yatolewayo
na PSSSF, Wastaafu wataweza kujihakiki kwa njia ya biometric, lakini pia elimu
kuhusu Hifadhi ya Jamii, jinsi ya kutumia huudma za PSSSF kiganjani, na taarifa
za uwekezaji.” Alisema Bw. Kolongo.
Maonyesho
hayo ambayo hufanyika kila mwaka, yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 23,
2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko na yatafikia
kilele Septemba 30, 2023.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 400.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...