Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MUUNGANO wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) umewashauri wabia wa Jukwaa la Mfumo wa Chalula Afrika( AGRF)kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kilimo, lengo likiwa  uzalishaji wa mazao ya chakula na tija kwa nchi za Afrika.

Ushauri huo umetolewa leo Septemba 5, 2023 jijini Dar es Salaam na Rais wa AGRA Dk. Kalibata wakati wa mkutano akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hussein Bashe baada ya kufanyika kwa ufunguzi uliofanywa na Makamu wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Hivyo wakati anazungumza ameomba wadau wa muungano huo wanachukua hatua kuhusu mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo huku akisisitiza hali ya hewa inajitokeza kama changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo katika Bara la Afrika.

Ameongeza hiyo inasababisha hali ya  kutotabirika  na isiyo na uhakika ya mifumo ya hali ya hewa katika bara la Afrika na hivyo  imeweka mzigo wa ziada kwa usalama wa chakula na maisha ya vijijini.

Ametoa mfano wa uharibifu wa mashamba na nyumba katika mafuriko ambayo yametoa karibuni  nchini Burkina Faso  huku pia akizungumzia ukame wa muda mrefu  Ethiopia."Hiyo inaonyesha ukubwa wa tishio linaloletwa na mabadiliko ya hali ya hewa Afrika."

Pamoja na hayo ameonesha kushangazwa namna za Kiafrika zilifanikiwa kufanya biashara na nchi za nje ya bara lakini zilifanya vibaya katika biashara ya ndani ya bidhaa za kilimo.

Amefafanua Afrika inanunu chakula kutoka nje ambacho wakulima wa Bara hilo  wanaweza kuzalisha. 

Awali Waziri Bashe amezungumzia kuhusu wakulima wadogo waweze kuboresha uzalishaji wanahitaji sera na miundombinu bora huku akieleza ushiriki mdogo wa vijana katika kilimo ulitokana na mtazamo ambao umejengwa kwenye simulizi la awali la kilimo.

Pia amesema Serikali ya Tanzania imeanzisha  mpango wa Ruzuku na Mikopo nafuu kwa vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili waweze kushiriki katika usindikaji na ufungashaji wa mazao ya kilimo.

Amefafanua vijana wanapoona wenzao katika kilimo wanafanikiwa nao watapenda pia kujishughulisha na kilimo lakini amesisitiza mazingira mazuri yanayowekwa kwenye kilimo yatahamasisha vijana wengi kujikita kwenye kilimo.

Waziri Bashe alitumia mfano wa vijana ambavyo wengi wao wameamua kujihusisha na usafiri wa bodaboda bila kuhamasishwa na mtu, ndivyo ambavyo kwenye kilimo nako inatakiwa ifike wakati vijana iwe ni kimbilio lao.

Pia amesema kwa mikakati iliyopo mkulima mdogo wa Tanzania atakuwa ni yule ambaye aanzia heka 10 na Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wananchi wengi wanajihusisha na kilimo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...