Na.Khadija Seif, Michuziblog 

BENDI Ya Mlimani park orchestra imetoa taarifa rasmi kuwa inatarajia kufanya Maadhimisho ya Miaka 45 tangu kaunzishwa kwa bendi hiyo pamoja na kuzindua Album mpya Septemba 30,2023 Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Michuziblog Mratibu mkuu wa mipango na matukio wa bendi hiyo Hassan msumari amesema bendi hiyo imejipanga vyema kuwapa burudani mashabiki wake kufatia ujio wa uzinduzi wa Album yao mpya yenye nyimbo takribani 8 zilizoshirikisha wasanii mbalimbali akiwemo mkongwe Hassan rehan bichuka, Mackey Fanta ambae ni ingizo jipya la bendi hiyo lengo ni kuchanganya ladha za wakongwe na kurithisha muziki wa dansi kwa vizazi vya sasa.

Hata hivyo  Msumari ameeleza maandalizi ya uzinduzi wa Album hiyo itasindikizwa na matukio mbalimbali huku Mgeni rasmi akitegemewa kutoka Wizara yenye dhamana ya Utamaduni,Sanaa na Michezo. 

"Tunategemea ugeni kutoka wizara yetu sikivu na tayari tumefanya mazungumzo na katibu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said yakubu na tunategemea ataitisha Mkutano na Wanahabari kabla ya siku ya Maadhimisho yenye .''

Wakati huo huo Kwa upande wake Meneja mradi kutoka Shirika la Maendeleo  (DDC) Fransic Hiza amesema wataendelea kushirikiana na bendi hiyo ya Mlimani park Orchestra kwani wanatambua mchango wao mkubwa katika kukuza na kuendeleza muziki wa dansi nchini. 


Hata hivyo Fransic ameeleza kuwa Ukumbi huo wa Magomeni Kondoa umekuwa ukiratibu shughuli mbalimbali za kimuziki hasa muziki wa dansi hivyo kutokana heshima ya bendi ya Mlimani park Orchestra uzinduzi na maadhimisho hayo yatafanyika ukumbi huo huo ili kuwaleta karibu mashabiki wa bendi hiyo kushuhudia burudani .


Pia ametoa rai kwa wanafanya kushirikiana na bendi za Muziki wa dansi kuhakikisha muziki huo unajitangaza zaidi na kupigwa kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...