Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Samia Suluhu Hassan amebainisha baadhi ya viashiria ambavyo vitathibitisha kufanikiwa kwa mpango wa kilimo wa BBT ambao umenzshwa na Serikali yake kwa kuwapatia fursa vijana kujihusisha na kilimo nchini kupitia mpango huo .

Akizungumza leo Septemba 7,2023 jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika(AGRF) Rais Samia ameeleza kwa kina baadhi ya viashiria ambavyo vitaonesha BBT.

Ametaja baadhi ya viashiria hivyo cha kwanza ni idadi ya vijana walio katika mpango huo ambao wapo zaidi ya  1200 lakini bado kuna maombi mengi kutoka kwa vijana kutaka kuingia katika huo mpango.

“Kwa hiyo  kiashiria cha kwanza ni vijana kuvutika na mpango wa BBT , lakini kiashiria cha pili kitakuwa kwa namna wanavyotumia mbolea katika kuzalisha , jinsi inavyotumika sana ndipo tutajua vijana wameelewa na wanafanya kilimo cha kisasa.

“Matumizi ya mbolea yatatupa kiashiria kwamba kuna matokeo chanya.Kiashiria kingine ni tija itakayopatikana katika kile ambacho vijana watakuwa wamehusika nacho,”amesema.

Rais Samia amesema kiashiria kingine ni soko kwa maana vijana watakavyopeleka hayo mazao sokoni na watakavyoendesha maisha yao huku akisisitiza kiashiria kikubwa zaidi ni kuona maisha ya vijana yanavyoendelea kustawi,

Ameongeza pia kufanikiwa kwa mpango wa BBT ni pale watakapoona wameshusha mfumuko wa bei ya gharama za chakula ndani ya nchi.

“Kama uzalishaji utakuwa mkubwa bila shaka bei za chakula zitashuka na kama tunavyojua mfumuko ndio unasababisha bei za chakula kupanda ndani ya nchi.

“Tukiweza kushusha mfumuko wa bei ya vyakula kitakuwa kiashiria kizuri sana kwamba vijana wanazalisha kwa wingi.”Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...