Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UWEPO wa mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika mwaka 2023 ambao unaendelea nchini Tanzania umetajwa kuwa na faida lukuki ikiwemo ya nchi kupata fedha za kigeni hasa Dola.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alipokuwa akielezea manufaa ya mkutano huo ambapo amesema moja ya changamoto iliyopo ni uhaba wa dola lakini uwepo washiriki zaidi ya 4000 kutoka mataifa mbalimbali maana yake kutakuwa na matumizi ya fedha za kigeni na hivyo kama nchi itanufaika na fedha hizo.

"Kufanyika Kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo hapa nchini kunaweza kusababisha kupunguza tatizo la dola ambalo limekuwepo kwani  Dola inapokuja nchini inapunguza tatizo hilo."

Amefafanua hata kwa  upande wa vyakula Tanzanaia itafaidika  ukiwemo mkoa wa Dar es Salaam."Dar es salaam ndio kila kitu na kuna wakazi si chini ya milioni tano na ndio kitovu cha masuala mengine yote yanayohusu biashara za kawaida za ndani na nje."

Ameongeza kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuja kwenye mkutano huo hadi ukumbi wa Mwalimu Nyerere unaonekana ni mdogo na sasa wanapata wazo la kufikiria  kuongeza kumbi zingine  na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaliona hilo

Akielezea zaidi kuhusu mkutano amesema kutokana na wingi wa wageni walioshiriki imefanya ukumbi wa Mwalim Nyerere kuonekana mdogo na sasa inawapa mawazo mapya ya kufikiria kuuongeza maeneo mengine nje ya ukumbi huo hasa kwa kuzingatia Tanzania imekuwa ikipokea mikutano mingi mikubwa.

"Baada ya mkutano huu wa AGRF kuna mkutano mwingine mkubwa wa  shirikisho la  michezo Duniani  ambao utafanyika nchini Tanzania na mambo yakiwa tayari Rais Dk.Samia Suluhu Hassan atatuongoza kuhusu mkutano huo."

Amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo yameanza na kwa wakazi wa Dar es Salaam ni fursa nyingine kwao katika kuwahudumia wageni hao.Kuhusu hali ya ulinzi na usalama amesema Dar es salaam iko salama na ulinzi uko wa kutosha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...