Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla amesema, Serikali imetoa kipaumbele kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuendeleza uchumi wa kidigitali.

Uchumi wa Kidijitali serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo wananchi wanahitaji huduma kwenye mkongo huo na kuona shirika hilo likifanya kazi yake kwa ufanisi unaotakiwa ili kutekeleza majukumu waliyonayo.

Abdulla ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukagua vifaa vya mradi vitakavyotumika katika upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano awamu ya tatu sehenu ya pili.

Amesema Serikali imemwamini Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga na ndio maana imemkabidhi kituo cha data na mkongo wa taifa kwa lengo la kuvifanyia kazi.

Katibu Mkuu huyo amesema mradi huo unatakiwa kumalizika kwa wakati kwa lengo la kuleta tija kwa wananchi kwa sababu fedha zinazotumika ni za watanzania.

Hata hivyo amesema taasisi za serikali ambazo hazijaingia Kituo cha Data ziingie kwani nafasi zipo za kutosha

“ Sitaki stori nyingi kwenye mradi huu nataka utekelezaji wa kazi na kazi lazima ifanyike kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa na mkandarasi ,”amesema Abdulla.

Hata hivyo katika ziara hiyo Katibu Mkuu alizihimiza Wizara na taasisi zingine ziweke taarifa zake katika kituo cha data cha TTCL.

Aidha aliwataka wakandarasi wa mradi huo wafanye wajibu wao kama mkataba wao ulivyotaja ili wananchi waweze kuanza kupata huduma hiyo kwa kutumia mkongo wa taifa

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Ulanga alisema Shirika hilo linaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha wilaya zote nchini zinaunganishwa na mkongo wa Taifa.

Mhandisi Ulanga alisema mradi wa awamu ya tatu unakwenda kutekeleza Wilaya 32, ambapo Wilaya 23 ziko chini ya Mkandarasi na Wilaya nyingine Tisa (9) ziko chini ya TTCL.

“Magari 44 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yameshapatikana na tayari yanatumika kwenye shughuli hizi ili kuongeza ufanisi zaidi katika mradi huo”,alisema

Mhandisi Ulanga alimuakikishia Katibu Mkuu kuwa, Menejimenti yake itasimamia miradi hiyo kwa ukamilifu,kwa weledi,pamoja na kukamilika kwa wakati .

“ Wasimamizi wa Mradi hakikisheni mnasimamia mradi kwa ukamilifu na kwa weledi. Changamoto zitakazojitokeza tafadhali ziwasilisheni mapema katika Menejimenti ili tuweze kuzifanyia kazi kwa ukaribu na haraka”,amesema.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Mohammed Khamis Abdulla  akipata maelezo kutoka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga wakati Katibu  Mkuu huyo alipitembelea na Kukagua vifaa  kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  wa awamu ya tatu sehemu ya pili , jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Mohammed Khamis Abdulla akizungumza mara baada ya  Kukagua vifaa  kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  wa awamu ya tatu sehemu ya pili , jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mameneja wa kusimamia ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
Sehemu picha ya mkandarasi wa kujenga sehemu ya mradi wa ujenzi Mkongo wa Taifa wa Mawsiliano jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...