Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Simba SC ya Tanzania itacheza dhidi ya Al Ahly SC ya Misri kwenye mashindano ya ‘Africa Football League’ (AFL) ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 20, 2023, ikiwa ni mchezo wa ufunguzi ambao utachezwa nchini kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mashindano hayo rasmi yanayoratibiwa na Shirikisho la Soka duniani (FIFA) na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) yatachezwa kwa muda wa wiki nne pekee, yakianza kati ya 20-25 Oktoba na kutamatika Novemba 5 na 11, 2023.
Mashindano hayo yatachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini (home and away) yakianza na timu nane (8) kubwa kutoka bara husika la Afrika, na yataanza hatua ya Robo Fainali kwa sababu ya timu shiriki nane (8) baadae yataingia kwenye Nusu Fainali na hatimaye Fainali.
Simba SC watacheza dhidi ya Al Ahly SC, Oktoba 20, 2023 ikiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Oktoba 24, 2023 nchini Misri.
Atlético Petróleos de Luanda ya Angola watacheza dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ikiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali, Oktoba 21, 2023 na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Oktoba 24, 2023.
Mchezo mwingine, Enyimba FC ya Nigeria watacheza dhidi ya Wydad AC ya Morocco, Oktoba 22, 2023 mchezo wa mkondo wa kwanza na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Oktoba 25, 2023.
TP Mazembe ya DR Congo watacheza dhidi ya Esperance de Tunisi ya Tunisia kati ya Oktoba 21, 2023 mchezo wa mkondo wa kwanza na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Oktoba 25, 2023.
Nusu Fainali ya mashindano hayo itachezwa kati ya Oktoba 29 ikiwa ni Nusu Fainali ya mkondo wa kwanza na Novemba 1, 2023 Nusu Fainali ya mkondo wa pili. Fainali itachezwa kati ya Novemba 5, 2023, Fainali ya mkondo wa kwanza na Novemba 11, 2023 Fainali ya mkondo ww pili.
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ametajwa kuchukua kitita cha zaidi ya shilingi Bilioni 27 (Tsh. 27, 555, 000, 000.00) huku kiasi cha Dola Milioni 2.5 ambayo ni zaidi ya shilingi Bilioni 5 zikitolewa kwa kila timu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...