Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati aliporipoti ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Kassim, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja Kamishna wa Dawa za Kulevya… Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako, Septemba 2, 2023.

*Ampongeza kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais, amuahidi ushirikiano

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Septemba 2, 2023 amemkaribisha Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiongezea nguvu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Mheshimiwa Dkt. Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu ili waweze kusimamia uratibu shughuli za Serikali kwa pamoja.

“…Kwa niaba yenu Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu tunakukaribisha sana hapa katika ofisi yetu na tunakupongeza kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kupewa jukumu kubwa la Naibu Waziri Mkuu kwa lengo la kusimamia shughuli za Serikali. Nakuhakikishia kwamba una timu imara ambayo inatoa ushirikiano wakato wote.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano. Amewaomba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wafanye kazi kwa bidii ili maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia na watanzania yaweze kufikiwa.

Viongozi wengine walioshiriki mapokezi hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.

Wengine ni Naibu Waziri Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Syprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu
Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko akisaini kitabu wakati wa mapokezi rasmi ofisini, yaliyofanyika kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijijini Dar es salaam, Septemba 2, 2023. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu alipomkaribisha ofisini Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam, Septemba 02, 2023 Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja Kamishna wa Dawa za Kulevya Aretas Lyimo, Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako Septemba 2, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...