Na Gift Thadey, Geita
GAVANA
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba amewasihi wachimbaji wa
madini nchini kutotembea na fedha taslim mifukoni badala yake watumie
mifumo ya kielektroniki katika kutoa na kupokea fedha.
Gavana
Tutuba ameyasema hayo Mjini Geita wakati akizungumza na waandishi wa
habari katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini.
"Nawashauri
wachimbaji kutumia mifumo ya kielelektoniki kupokea na kutoa fedha
badala ya kutembea na fedha taslimu," amesema Tutuba.
Gavana
Tutuba amesema wao kama BOT wanalipa kwa mfumo wa TIPS ambao
unarahisisha kwa kuwa umeunganishwa na mabenki yote na miamala ya simu
nchini.
"Ndiyo sababu tunawahamasisha wachimbaji watumie mifumo
ya kielektroniki kuliko fedha taslimu kwa kuwa ni mfumo wa haraka na una
nafuu utawaepusha na fedha bandia," amesema Gavana Tutuba.
Amesema
kuwa na mfumo wa kielektroniki ni nafuu zaidi hata kuepuka kuibiwa
fedha tofauti na kuwa na fedha taslimu mkononi au mfukoni.
Gavana
wa Benki Kuu (BOT) Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari
Mjini Geita kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya
madini. Picha na Gift Thadey
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...