Pemba – Wajasiriamali wanawake 30 kutoka Pemba, leo wamehitimisha mafunzomaalumu ya wiki 13 katika biashara na ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Serikali yaMarekani kupitia kupitia programu yake ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wanawake(Academy of Women Entrepreneurs – AWE).

Balozi wa Marekani nchini Dk. Michael Battle aliwapongeza wanawake hawa akiwahimiza kutumia mafunzo waliyoyapata kuendelea kujenga biashara zenye mafanikio. Mahafali haya yaliyohudhuriwa pia na

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar – Mhe Mudrick Ramadhan Soraga, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Salama Mbarouk Khatib, Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Mhe. Abdalla Rashid Ali, Mratibu wa Maktaba ya Taifa Pemba Bw. Ahmed Amour, na wageni wengi wengine waalikwa. 


AWE ni mpango wa Kimataifa wa Serikali ya Marekani wa kuwawezesha wanawake kiuchumi unaokusudia kuwajengea uwezo wanawake milioni 50 duniani kote kufikia upeo wa uwezo wao kiuchumi. AWE ina dhamira ya dhati ya kuwapa wanawake elimu na ujuzi, kuwajengea mitandao na kufungua fursa wanazohitaji ili kuyabadilisha mawazo yao kuwa miradi halisi ya kujiletea kipato.


Akizungumza na wahitimu katika mahafali hayo, Balozi Battle alielezea matokeo ya mafunzo yanayotolewa na AWE. “Mafunzo ya wiki 13 mliyoyapata mkiwa sehemu ya programu hii yamewapa ujuzi kwa vitendo utakaowawezesha kuanzisha biashara endelevu pamoja na kuwaunganisha na wakufunzi (mentors) na wajasiriamali kama ninyi

wa nchini Marekani,” alisema.


Aliendelea kusema kuwa kuwajengea wanawake uwezo wa kiuchumi ndio njia ya haraka zaidi ya kuibadilisha jamii. “Jitihada za wanawake huwa na matokeo makubwa zaidi kwa jamii nzima kwa sababu wanawake wanapofanikiwa mara nyingi watawekeza mapato yao katika familia na jamii zao, wakigharamia mahitaji kama vile ada kwa watoto wao na huduma za afya.  Manufaa ya kiuchumi ya mafanikio yenu yanasaidia vizazi vijavyo.Tayari ubunifu wenu unaleta matokeo chanya katika jamii na uchumi wa Tanzania,” alisema.


Kundi la wahitimu wa Pemba ni kundi la kumi la washiriki wa programu ya AWE. Makundi mengine ya wanawake walioshiriki katika programu hii ni kutoka Dar es Salaam, Iringa, Zanzibar, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Bagamoyo, Kigoma, na Kagera. Kupitia Ubia na Taasisi ya Marekani ya Maendeleo ya Afrika (U.S. African Development Foundation -USADF), wajasiriamali wanaoshiriki programu ya AWE wanaweza kupatiwa na USADF fedha za mtaji wa hadi Dola za Kimarekani 20,000 ili kupanua biashara zao.


Ubalozi wa Marekani unashirikiana na Selfina kutekeleza programu ya AWE nchini Tanzania. Ikiwa imeanzishwa mwaka 2002 na Dk. Victoria Kisyombe, Selfina ni taasisi ya Kitanzania ya utoaji mikopo midogo midogo iliwalenga zaidi akina mama wajane na wasichana. Katika miaka 19 iliyopita, Selfina imewawezesha kiuchumi zaidi ya

wanawake 31,000 kupitia mikopo inayozunguka. Maisha ya zaidi ya watu 300,000 yamegushwa kutokana na faida zilizopatikana kutokana na mikopo hiyo. Wanawake sasa ni wamiliki wa biashara zao wenyewe na zaidi ya nafasi za ajira 150,000b zimetengenezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...