Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

WASHIRIKI kwenye  kongamano la saba la uwezeshaji wananchi Kiuchumi litafanyika Jijini Dodoma  mwezi huu Septemba 29 pamoja na mambo mengine watathmini utekelezwaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa amesema tangu kuanzishwa kwa sera ya uwekezaji hapa nchini utekelezaji wake umegusa maisha ya watanzania wengi katika kada mbalimbali sambamba na kupunguza umaskini miongoni mwa watanzania.

 

“Kongamano la hili ni muhimu sana katika sekta au tasnia ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwani ni kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan,” alisema Bi. Issa.

 

Akizungumza na waandishi wa hapa jijini hapa jana mbali ya kutathmini utekelezaji wa sera ya uwezeshaji ambayo mpaka sasa imeonyesha mafanikio makubwa kwenye utekelezwaji wake ikiwemo kubadilisha maisha ya watanzania wengi na  kutoa mchango stahiki kwa maendeleo kiuchumi na kijamii.

 

“Kauli Mbiu ya Kongamano hilo la saba ni ‘Uwezeshaji kwa Uchumi Endelevu’ kwani inatoa fursa ya kujadili kwa kina masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa uchumi endelevu wa Tanzania,” alisema.

 

Alisema katika kuonyesha umuhimu wa kongomano hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza alisema Kongamano litaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Mb) ambalo litatanguliwa na wiki ya uwezeshaji pamoja na maonesho ya siku tatu ya wajasiriamali yatakayoanza septemba 26 hadi 28 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

 

 “Ikumbukwe kuwa  kwenye kongamano la sita ,Waziri Mkuu Majaliwa aliwaagiza wakuu wa mikoa yote kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi,” alisema Bi. Issa na kuongeza kuwa dhamira ya Rais Dkt.Hassan ni kuona kila mtanzania anafaidika na sera ya uwekezaji.

              

Tuzo mbalimbalin zitatolewa kwa wote waliofanya vizuri ikiwemo mkoa uliofanya vizuri, wajasiriamali na taasisi  mbalimbali za uwezeshaji  kwani mafanikio mengi yameshapatikana chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

Kongamano litawashirikisha Wizara, Mashirika, Wakala na Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Mikoa, Halmashauri, Wajasiriamali, Taasisi za Fedha, Taasisi za Elimu, Tafiti, Wawekezaji pamoja na wadau wengine wa masuala ya uwezeshaji.

Bi. Issa  alichukua fursa hiyo kuwakaribishwa watanzania wote kujionea na kujifunza masuala mazima ya uwezeshaji, upatikanaji wa mitaji, fursa zilizopo kwenye miradi ya mkakati,masoko na hata kutengeneza mtandao wa watu, Taasisi au Kampuni ya kujiendeleza kiuchumi

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC),Bi. Beng'i Issa akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma jana kuhusu Kongamano la Uwezeshaji wananchi kiuchumi litakalofanyika Septemba 29 mwaka huu Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...