*Wahandisi na Makandarasi wawatumie katika miradi
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema kuwa katika miradi ya ujenzi inayotekelezwa nchini kwa Wakandarasi kutumia mafundi wenye ujuzi ambao wamehitimu katika vyuo vya VETA.
Hayo ameyasema Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha kwenye Maonesho na Mkutano Mkuu wa 20 wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (ERB)yaliyofanyika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Dora amesema wahitimu wa VETA ni mafundi wenye ujuzi ambapo wanaweza kufanya kazi na kuwarahisishia Wahandisi na Wakandarasi kuwa mafundi walionao wameiva.
Aidha amesema kuwa baadhi ya vijana waliohitimu VETA wako katika kampuni mbalimbali na mrejesho wake wa katika kazi ni mzuri na kutaka vijana waende katika vyuo vya VETA kupata ujuzi.
Amesema kuwa Vyuo vya VETA vimejengwa kila Wilaya ambapo vijana waende kupata mafunzo ya ufundi Stadi na ambao wanafanya kazi za ufundi bila kuwa na mafunzo VETA inachukua na kuwatambua kwa kuwapitisha programu maalumu ya Wanagenzi.
Mwanafunzi wa VETA Chang'ombe fani ya Fundi bomba Kebori Mwita amesema VETA ni mkombozi kwake kwani ana uhakika wa kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri kutokana mahitaji mafundi bomba.
Amesema kuwa vijana watumie fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwani ni uhakika wa kupata kazi moja kwa moja ya kujiajiri ambapo haijawahi kutokea fundi akakosa kazi.
Kwa upande wa Mwanafunzi wa Chuo hicho Fani ya Useremala Nuru Ally amesema kuwa amechagua fani hiyo kutokana na kuipenda kwa kuamini itamsaidia katika ajira ya uhakika pia wasichana wa kike wanaikimbia hivyo yeye anafungua milango.
Mwanafunzi wa Fani ya Ufundi Bomba Kebori Mwita akizungumza fani ya Fani hiyo kwenye fursa ya ajira kwenye maonesho na Mkutano Mkuu wa 20 wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (ERB) jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha akizungumza na waandishi wakati wa maonesho na mkutano wa 20 wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...