Na Shalua Mpanda-TMC

MANISPAA  ya Temeke mkoani Dar es Salaam imeendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo Meya Abdallah Mtinika amekutana na wataalamu wa Taasisi ya Tomorrow 's Cities kutoka Uingereza.

Lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati na kujenga uelewa wa namna jinsi ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yakiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua za El-nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Temeke , Mtinika amesema wanatarajia kufanya kikao kikubwa Septemba 28 mwaka huu ambapo wawakilishi wengine kutoka nchi mbalimbali watashiriki.

"Lengo kuu la mkutano huu ni kufanya Utafiti utakaosaidia wanatemeke kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa mafuriko na pia upangaji wa miji, " amesema Meya Mtinika

Taasisi hiyo ya Tomorrow 's Cities itafanya Utafiti huo kwa kipindi cha miezi sita  ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam ambapo itabaini changamoto zote zinazosababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake Mtaalam kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es salaam Profesa Willbard Kombe amesema umuhimu wa Utafiti huu ni kwamba utasaidia kutambua ukubwa wa maafa na namna ya kuweza kukabiliana na maafa hayo.

Mwakilishi kutoka taasisi ya Tomorrow 's Cities  UCL,Bw.Mark Pelling amemshukuru Meya Mtinika kwa kuwaalika kufanya Utafiti huo katika wilaya ya Temeke na kusema kuwa Utafiti huu utaleta matokeo chanya na kuweza kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo wa ufunguzi pia umewakutanisha maofisa ardhi na mipango miji kutoka manispaa ya Temeke pamoja wataalamu wengine.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...