Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) ametoa wito kwa Watanzania kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta ya kula hususan alizeti kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya uzalishaji wa mafuta ya kula nchini na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa malighafi hiyo kwa uzalishaji wa mafuta ya kula kwa mwaka mzima.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Septemba 12, 2023 alipofanya ziara katika Kiwanda cha mafuta ya kula ya Korie na Sundrop pamoja na sabuni cha Wilmar Tanzania Limited, na Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes) vilivyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto.

Akiwa katika Kiwanda cha mafuta ya kula ya Korie na Sundrop pamoja na sabuni cha Wilmar Tanzania Limited, Dkt. Kijaji amewahakikishia Watanzania kuwa Kiwanda hicho kinaagiza mafuta ghafi na kuyachakata kupata mafuta ya kula na mabaki hutengenezwa sabuni. Bidhaa hizo huuzwa katika soko la ndani na nje hususani katika soko la EAC na SADC.

Akiwa katika Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes), Dkt. Kijaji amewashauri Watanzania kununua na kutumia bidhaa zinazalishwa nchini ili kuendelea kuzalisha ajira na kukuza pato la Taifa hususani fedha za kigeni.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametembelea Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes) kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo, Jeti, jijini Dar es Salaam, Septemba 12, 2023

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...