· Ushirikiano huu ambao umepewa nguvu na TripSiri unaendeleza dhamira ya Vodacom ya kuekelea dunia ya kidigitali

Vodacom M-Pesa na Precision Air waemingia ushirikiano ambao utawawezesha wateja kukata tiketi ya ndege kupitia applikesheni ya M-Pesa Super App na kufurahia punguzo la bei mpaka 20% kwa bei ya tiketi ya kawaida. Ushirikiano huo umepewa nguvu na TripSiri, kampuni ya usafiri na teknolojia ya Tanzania ambayo inalenga kurahisisha huduma ya ukataji wa tiketi kupitia M-Pesa Super App.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni amesisitiza suhirikiano huu unaonyesha kujizatiti kwao kuifanya M-Pesa kuwa sehemu ya Maisha ya kidigitiali ya kila mtu ikiwezesha manunuzi na malipo ya bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na Watanzania katika maisha yao ya kila siku zinapatikana kwenye simu zao za mkononi.

“Tunayo furaha kuwakaribisha Precision Air kujiunga na familia ya watoa huduma wanaokaribia 20 katika mtandao wetu mpana wa M-Pesa. Kupitia ushirikiano huu, wateja hawatohitajika tena kutembelea ofisi au tovuti zao kwa ajili ya kukata tiketi za ndege. Tumewarahisishia zoezi hilo na sasa wanaweza kufanya hivyo kwa kupitia aplikesheni ya M-Pesa inayopatikana katika simu zao za mkononi. Kwa kuongezea, watanufaika na punguzo la 20% kwa kukata tiketi ikiwa ni faida ya kutumia mtandao wetu. 

Malengo yetu ni kuwajengea wateja na Watanzania utamaduni wa kufanya malipo na manunuzi yao kwa usalama na uharaka pamoja na kuwarahisishia kutunza kumbukumbu zao za kifedha kwasababu kupitia M-Pesa unaweza kuzipata taarifa zote za manunuzi unayoyafanya,” alielezea Bw. Mbeteni.

M-Pesa imeleta mapinduzi katika manunuzi na malipo ya huduma na bidhaa kutoka kwa mamia ya wafanyabiashara mbalimbali Tanzania kupitia simu za mkononi.

 Tangu kuanza kuwahudumia Watanzania kwa miaka 15 sasa, imekuwa ni chachu katika maendeleo ya shughuli za kibenki na kifedha na kupunguza pengo kwa watu ambao bado hawajaunganishwa na mifumo hiyo.

Bw. Mbeteni aliongezea kuwa, “mbali na kuwezesha malipo, pia tunalenga kuwarahisishia wafanyabiashara shughuli zao kwa kuwaleta karibu zaidi na wateja. Jukwaa la M-Pesa limekuwa kama soko ambalo mteja akiingia ana uwezo wa kuchagua mahitaji yake ya siku, akalipia, akatoka na kuendelea na shughuli zake zingine.

 Teknolojia imekuja kuondoa adha ya watu kuepukana na kutembea umbali mrefu na kupoteza muda ambao wangeuwekeza katika shughuli nyingine shukrani kwa washirika wetu kama vile TripSiri ambao wamelifanikisha hili. Tutaendelea kutumia fursa zinazotokana na ushirikiano kama ambao tumeutangaza leo kama njia mojawapo ya kuongeza huduma na bidhaa nyingi zaidi. 

Tunatumaini kama taifa, hivi karibuni tutafikia hatua ambayo mtu hautohitaji kuwa na pesa taslimu ili kuhudumiwa sehemu yoyote.”

Kwa upande wake Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Precision Air, Hillary Mremi alisema kuwa, “tunajivunia kufanikisha ushirikiano wetu na M-Pesa, huduma ambayo imekuwa ikitumiwa na kuaminiwa na Watanzania kwa muda mrefu. Kujiunga kwetu na familia hii kutawarasishia wateja wetu na zaidi ya milioni 17 ambao wamo tayari ndani ya mtandao huu kutosumbuka tena kuja ofisini kwetu au kutembelea tovuti ndipo wakate tiketi ya ndege. 

Ningependa kuchukua fursa hii kuwahikikishia kuwa huduma ambayo wataipata katika mtandao huu ni sawa ambayo watakuja katika ofisi zetu. Maana kumekuwepo na hofu kwamba mteja anaweza akakata tiketi kisha akakataliwa kusafiri. Suala hilo si la kweli kwasababu kilichobadilika hapa ni urahisi wa upatikanaji wa huduma zetu.”

Kwa kumalizia Mkurugenzi wa TripSiri, Bw. Gaurav Dhingra alimalizia kwa kusema, “Tumefurahi kushirikiana na Vodacom M-Pesa kutumia teknolojia yetu na uzoefu katika sekta ya usafiri kuwarahisishia zaidi huduma wateja wa M-Pesa na Precision Air. 

Huu ni mwanzo tu wa kufanikisha dhamira yetu ya kuleta mabadiliko ya sekta ya usafiri wa anga nchini Tanzania kwenye Nyanja tofauti, na ushirikiano huu ni hatua nzuri ya mwelekeo wan jia tunayokwenda.”

Ukiachana na urahisi na usalama wa kutuma na kutoa pesa katika aplikesheni ya M-Pesa mteja amewezeshwa kufanya malipo na manunuzi ya huduma mbalimbali zikiwemo usafiri, ada, faini, maji, LUKU, ving’amuzi, malipo ya serikali, bima, mafuta, na nyinginezo nyingi zaidiMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...