Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Usafirishaji wa Wizara hiyo waliostaafu kazi hivi karibuni, ambapo aliwashukuru watumishi hao kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote walipokuwa kazini. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, akimkabidhi zawadi ya pongezi kwa Afisa Usafirishaji Mstaafu wa Wizara hiyo, Bw. Issa Abdallah (kushoto), kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote alipokuwa kazini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa hao waliostaafu kazi hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi, Jenifa Omolo, akikabidhi zawadi ya pongezi kwa familia ya Afisa Usafirishaji Mstaafu wa Wzara hiyo, Bw. Enock Macha, kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili muda wote alipokuwa kazini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa hao waliostaafu kazi hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakicheza na kufurahia wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Usafirishaji wa Wizara hiyo walistaafu kazi hivi karibuni, iliyofanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na familia za ya Maafisa  Usafirishaji wa wizara hiyo waliostaafu kazi hivi karibuni, Bw. Issa Abdallah (wa tatu kulia) na Bw. Enock Macha (wa pili kulia), baada ya hafla fupi ya kuwaaga, iliyofanyika katika Hoteli ya Royal Village, jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...