Na Shalua Mpanda -TMC

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jaffo amefurahishwa na utendaji kazi wa viongozi wa wilaya ya Temeke katika suala la usafi wa mazingira.

Ameyasema hayo leo Septemba 19,2023 wakati wa kampeni maalum ya usafi katika eneo la Mbagala Zakhem ambapo alishiriki kusafisha mitaro na mifereji katika kujiandaa na mvua za El-nino zinazotarajia kuanza hivi karibuni.

Waziri Jafo amesema hali ya usafi hasa katika barabara kuu ya Kilwa aliyoikuta Leo ni tofauti na aliyokutana nayo kipindi cha nyuma ambapo alitoa maagizo kwa viongozi hao ambao kwa kiasi kikubwa wametekeleza.

"Kwa kweli mkuu wa wilaya naomba niseme ukweli,hii barabara imebadilika ni safi,na hii inaonesha "leadership"(uongozi) wa Temeke ulivyo."

Aidha ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia usafi katika maeneo yao na kuhamasisha Wananchi kufanya usafi katika makazi yao.

Wakati huo huo mkuu wa wilaya ya TemekeMobhare Matinyi amekutana na watendaji wa Kata,Mitaa,maafisa Afya na Mazingira wa manispaa hii katika kikao kilichokuwa na lengo moja tu la kufanya na kusimamia usafi katika maeneo yote ndani ya manispaa ya Temeke.

Matinyi amewaeleza viongozi hao wa mitaa pamoja na maafisa Afya kuwa jukumu la kusimamia usafi ni la kila mmoja,hivyo wanapaswa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ili kuweza kuepukana na uwezekano wa kutokea mafuriko pindi mvua hizo zitakapianza.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa hii Elihuruma Mabelya ni muendelezo wa mikakati ambayo viongozi wa Manispaa wamejiwekea kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ambapo Mkuu wa wilaya ametangaza wiki mbili zaidi za kampeni za usafi mara baada ya wiki ya kwanza ya usafi kukamilika Jumamosi iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...